Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limewaua
majambazi watatu mara baada ya
majibizano ya risasi yaliyotokea jijini
humo.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam,
Lazaro Mambosasa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo
amesema kuwa bado wanawasaka majambazi wengine wawili waliofanikiwa
kutoroka.
”Jeshi la polisi limewaua majambazi watatu katika majibizano ya
risasi, lakini kuna wengine walifanikiwa kukimbia lakini bado tunawasaka
mpaka tuwapate, ni lazima tukomeshe ujambazi katika kanda yetu,”amesema
Kamanda Mambosasa
No comments:
Post a Comment