Pages

Friday, May 3, 2019

MWILI WA DKT. REGINALD MENGI KUWASILI NCHINI JUMATATU MEI 6, 2019



MWILI wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dkt. Reginald Mengi utawasili nchini Jumatatu 6, 2019 na ndege ya Shirika la ndege la Emirate ukitokea Dubai, Falme za Kiarabu, Mwanasheria wa familia ya Dkt. Mengi, Bw. Michael Ngalo amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mei 3, 2019.
Mwili wa Dkt. Menghi ambaye alifariki dunia akiwa huko Dubai usiku wa kuamkia Mei 2, 2019, ukishawasili jijini Dar es Salaam, utahifadhiwa kwenye hospitali Kuu ya Jeshi, Lugalo na siku inayofuata yaani Jumanne Mei 7, 2019, shughuli ya kuaga mwili huo itafanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini.
Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa baada ya shughuli hiyo ya kutoa salamu za mwisho, mwili wa Dkt. Mengi utasafirishwa Jumatano Mei 8, 2019 kuelekea mahala alikozaliwa Machame, Mkoani Kilimanjaro ambapo shughuli za mazishi zitafanyika Alhamisi Mei 9, 2019.

No comments:

Post a Comment