Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt.
Faraja Mnyepe (wa tatu kulia) na Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Mazingira wa
Uganda Alfred Ollot wakionesha hati za makubaliano baada ya kusainiwa kwenye
Mkutano wa Kuendeleza Mahusiano ya Mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na
Uganda kwa ajili ya kurahisisha masuala ya kijamii, kiuchumi na kimazingira
uliomalizika juzi Bukoba mkoani Kagera. Wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu Wizara
ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dorothy Mwanyika na wa pili kulia ni
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki Dkt. Faraja Mnyepe (wa tatu kulia) na Katibu Mkuu Wizara ya
Maji na Mazingira wa Uganda Alfred Ollot (Wa pili kushoto) wakisaini Makubaliano
yaliyofikiwa katika mkutano wa Kuendeleza Mahusiano ya Mpaka wa Kimataifa kati
ya Tanzania na Uganda kwa ajili ya kurahisisha masuala ya kijamii, kiuchumi na
kimazingira uliomalizika juzi Bukoba mkoani Kagera. Wa kwanza kulia ni Katibu
Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dorothy Mwanyika na wa pili
kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt.
Faraja Mnyepe akizungumza wakati wa kuhitimisha Mkutano wa Kuendeleza Mahusiano
ya Mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Uganda kwa ajili ya kurahisisha
masuala ya kijamii, kiuchumi na kimazingira juzi Bukoba mkoani Kagera. (wa pili
kushoto) ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Mazingira wa Uganda Alfred
Ollot. Wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dorothy Mwanyika na wa pili kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo
na Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel.
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Makatibu Wakuu ukifuatilia Mkutano wa Kuendeleza Mahusiano ya
Mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Uganda kwa ajili ya kurahisisha
masuala ya kijamii, kiuchumi na kimazingira uliomalizika juzi Bukoba mkoani
Kagera.
Balozi wa Tanzania nchini Uganda Dkt Aziz Mlima akizungumza kwenye Mkutano wa Kuendeleza Mahusiano ya
Mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Uganda kwa ajili ya kurahisisha
masuala ya kijamii, kiuchumi na kimazingira uliomalizika juzi Bukoba mkoani
Kagera.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt.
Faraja Mnyepe (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na Washiriki wa Mkutano wa Kuendeleza
Mahusiano ya Mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Uganda kwa ajili ya
kurahisisha masuala ya kijamii, kiuchumi na kimazingira uliomalizika juzi
Bukoba mkoani Kagera (wa pili kushoto) ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na
Mazingira wa Uganda Alfred Ollot. Wa
pili kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dorothy Mwanyika na wa kwanza
kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Elisante Ole
Gabriel. (PICHA ZOTE NA MUNIR SHEMWETA
WA WIZARA YA ARDHI)
Na Munir Shemweta, BUKOBA
Mkutano wa Kuendeleza Mahusiano
ya Mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Uganda kwa ajili ya kurahisisha
masuala ya kijamii, Kiuchumi na Kimazingira umemalizika Bukoba mkoani Kagera
kwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt
Faraja Mnyepe na Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Mazingira wa Uganda Alfred Ollot
kusaini makubaliano yaliyofikiwa.
Mkutano huo wa siku
mbili ulimalizika juzi na kuwakutanisha Makatibu Wakuu wa nchi za Tanzania na
Uganda kutoka Wizara zinazoshughulika na masuala ya Ardhi Nyumba na Maendeleo
ya Makazi, Mambo ya Nje, Mifugo na Uvuvi, Maji pamoja na Nishati.
Kabla ya mkutano huo,
Wataalamu wa sekta zinazohusika kutoka nchi hizo mbili walikutana na
kujadiliana namna bora ya kukabiliana na changamoto zinazozikabili nchi za
Tanzania na Uganda katika eneo la Mpaka na baadaye kuwasilisha mapendekezo kwa
Makatibu Wakuu kwa lengo la kujadiliwa kwa manufaa ya nchi hizo.
Baadhi ya mambo
yaliyojadiliwa kwenye mkutano huo ni pamoja na Uimarishaji na Uthamini wa Mpaka
wa Kimataifa wa Tanzania na Uganda, Mpango Kabambe wa Utunzaji Mto Kagera na
Matumizi Endelevu ya Rasilimali za Bonde la Mto Kagera kati ya Tanzania na Uganda.
Akizungumza baada ya
mkutano huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel
alisema katika siku mbili za mkutano huo, nchi washiriki zilijadili namna bora ya
kuendeleza mahusiano ya mipakani kwa lengo la kurahisisha mambo ya kiuchumi,
kijamii na kimazingira sambamba na kujadili jinsi ya kuboresha matumizi endelevu
ya Rasilimali za Bonde la Mto Kagera ili ziweze kuleta manufaa kwa nchi za
Tanzania na Uganda.
Kwa upande wake Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maji na Mazingira wa Uganda Alfred Okidi Ollot alisema,
mkutano huo ni njia sahihi ya kuonesha kuimarika kwa mahusiano ya Tanzania na
Uganda na kusisitiza kuwa kilichofanyika ni kuonesha uhalisia wa ushirikiano kwa
lengo la kuwafanya wananchi wa pande
zote kunufaika.
Katibu Mkuu wa Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Faraja Mnyepe alizishukuru
pande zote mbili za nchi za Tanzania na Uganda kwa kufanikisha kufikiwa makubaliano
aliyoyaeleza kuwa yana lengo la kuleta manufaa kwa nchi za Tanzania na Uganda.
No comments:
Post a Comment