Pages

Thursday, May 2, 2019

KIFO CHA DKT REGINALD MENGI: SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZAENDELEA KUMIMINIKA”



Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umeandika kwenye ukurasa wake wa Instagram, "Tamko kufuatia kifo cha Reginald Mengi 2 MEI 2019, Ubalozi wa Marekani umepokea kwa majonzi makubwa taarifa ya kifo cha Reginald Mengi asubuhi ya leo, Tulipata fursa ya kufanya kazi na Dk.Mengi katika siku zilizopita, na kwahakika mchango wake katika ukuaji wa muda mrefu wa uchumi na maendeleo ya Tanzania ni mkubwa na muhimu mno. Tunatoa pole na rambirambi zetu za dhati kwa familia na rafiki zake na kuungana na watu wa Tanzania katika kuomboleza msiba huu mzito."


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameandika kwenye ukurasa wake wa tweeter, Moja ya vitu ulivyotuachia ni ule wepesi wako wa kusaidia masuala ya kijamii, daima tutakukumbuka. #RIPReginaldMengi

Alvaro Rodriguez, Mwakilishi Mkazi wa UNDP hapa nchini, ameandoika kwenye ukurasa wake wa tweeter, Very saddened to hear about the passing away of @regmengi. @UnitedNationsTZ joins #Tanzania in mourning his death. Our thoughts & prayers are with his family. May his soul rest in peace.
Samwel Nyalla, Mkurugenzi wa Sahara Media Group ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook
“Nimepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa ya kifo cha Rafiki yangu wa karibu mbia na mwanatasinia mwekezaji mzalendo na muumini wa kweli wa uhuru wa vyombo vya habari mmbunifu mwanzilishi na mpenda maendeleo Mzee Reginald Mengi Mungu ampokee na amuweke mahari pema peponi kwa niaba ya Kampuni ya Sahara Media Group Limited Basic Transimision Ltd na MOAT natoa salaam za rambi rambi kwa jamaa wanatasinia familia na watanzania wote waumini wote wa uhuru wa habari duniani kote tumepoteza jembe na kielelezo cha uzalendo na ubunifu mkubwa hapa nchini .Tuna kazi kubwa imeachwa ya kuziba hili pengo jambo ambalo si rahisi kwa lika hili tulilonalo ila Mungu ndiye tegemeo la wote tulimpenda sana yeye kampenda zaidi umetangulia kwake ila wote tutakufuata Mungu awe nasi daima Amen.

Zitto Kabwe Ruyangwa, Mbunge wa Kigoma Mjini, ameandika kwenye ukurasa wake wa tweeter, “Msiba mkubwa kwa Taifa na haswa kwa familia ya Mzee Mengi @regmengi, Pole sana @JNtuyabaliwe na watoto, The tweens, Poleni sana Regina. Abdiel na familia nzima ya makampuni ya IPP. Bwana ametoa na Bwana ametwaa.Mungu ailaze roho ya Mzee Mengi mahala pema anapostahili.”

Nape Nnauye, Mbunge wa Mtama ameandika kwenye ukurasa wake wa tweeter, “Umeacha alama kubwa! Nimejifunza mengi kwako, Rafiki, Mshikaji, Kiongozi na Mzazi! Ulinifundisha kuwa KUKATA TAMAA NI DHAMBI! {Msalimie Mzee Sitta, mkumbushe kile kikao chetu Cha mwisho nyumbani kwako}Pumzika kwa Amani Dr. R.A Mengi.
Cloudstv wameandika kwenye ukurasa wao wa Instagram, tumepoteza Baba (Dkt. Reginald Mengi), ambaye kila akija mjengoni hutupa moyo na kusema watoto wangu msiogope Baba yenu nipo nanyi kwenye kila hatua, Leo Baba kaenda nani wa kutunyamazisha, mara nyingi hutuambia sisi ni furaha yake tuzidi kufanya kazi lakini leo hayupo, @josephkusaga analia, Sheba Kusaga analia na wafanyakazi wa Clouds Media nao wanalia kwani Baba kaenda . Hatutamuona tena lakini tunaomba awasalimie wapendwa wetu Ruge Mutahaba pamoja na Kibonde, sisi tunazidi kuwaombea.
#TutaonanaBaadae


Benjamin Kasenyenda Andongolile, Mwandishi wa habari, ameandika kwneye ukurasa wake wa Facebook,Kweli kifo hakinaga huruma.Nimejiuliza sana je hivi kwanini kipo?Je kwanini tunaondoka huku duniani? Hivi kwanini maamuzi yasipitishwe huko juu kwamba sasa imetosha, kifo kiondoshwe tu....Swali hili pamoja na mengine kadhaa majibu yake anayo Muumba wetu pekee.Yetu sisi ni masikitiko, hasa pale tunapoondokewa na wale tuliowapenda sana.


Tangulia Mzee Mengi.Nenda.Tuko nyuma yako.Watanzania tunaumia sana maana tunabakiwa na maswali mengi yasiyo na majibu hasa pale tunapokumbuka mengi uliyotenda kwenye taifa hili. Mzee Mengi tutakukumbuka kwa mambo mengi kama lilivyo jina lako.Mzee Mengi kweli uligusa wengi.R.I.P
January Makamba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulikia Mazingira na Muungano, ameandika kwenye ukurasa wake wa tweeter “Poleole kwa Jacqueline na Regina, Abdiel and the twins - na familia nzima ya IPP Group. Mungu ailaze roho ya Mzee Reginald Mengi peponi”.

Shirika la Umeme Nchini TANESCO imeandika kwenye ukurasa wake wa Instagram, “TANESCO imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi, kilichotokea Dubai usiku wa kuamkia leo Mei 02, 2019. TANESCO itamkumbuka Dkt. Mengi kwa mchango wake mkubwa katika kuendeleza sekta ya nishati ya umeme kupitia viwanda na makampuni ya IPP na mchango wake mkubwa kwa jamii.
Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi. Amen
Haji Manara, Msemaji wa Klabu ya Simba, ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram Tarehe kama ya leo Mwezi mmoja tu uliopita yaan April ya mwaka huu pale Serena hotel mida ya saa moja usiku tulikuwa na Mwenyeki Mtendaji l wa Makampuni ya IPP Mzee wetu Reginald Abraham Mengi, naamka asubuhi hii naambiwa Mzee Mengi ameafariki !! Daaah so sad Wallah !!
Tulipokutana nae pale Serena aliniambia mambo mengi, ila nalikumbuka moja, huku akininong’eneza’ Mwanangu ww ni miongoni mwa vijana maarufu nchini ila umaarufu mzuri ni lazma uwe unaweza kusaidia watu kiuchumi,so hangaikia na pesa ‘ Wallah sijui why Mzee wangu aliniambia hvyo?
Ohhh God!! Twajua kazi yako huwa haina makosa but turuhusu kwa unyenyekevu tumlilie Baba na Rafiki yetu mpendwa, wenyewe tulikuwa tukimuita Chairman!! Rest In Peace Baba Mengi.
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abass, ameandika kwenye ukurasa wake wa tweeter. Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mwenyekiti wa IPP, Mzee Reginald Mengi. Kama alivyopata kusema yeye mwenyewe siku za uhai wake kuwa watu wanaoacha alama hawafi, basi mawazo, falsafa, ubunifu na kujitoa kwake vitaendelea kuishi nasi.”
Mohammed Dewji MO, ameandika kwenye ukurasa wake wa tweeter “Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un. Mwenyezi Mungu ampe pumziko na ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Ameen #RIPMengi
Bi. Leila Shekh, Mwenyekiti mstaafu wa TAMWA, ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook,Mzee Reginald Mengi Always in our hearts Pioneer of privately owned media houses in the URT. Gender Rights supporter.


Simon Mkina, Mwandishi wa habari ameandika kwenye ukurasa wake wa tweeter.Uliniita ofisini kwako miaka 24 illiyopita. Tukanywa chai. Tukapiga soga. Sikuondoka "mtupu." Mwaka juzi ukaniita nyumbani kwako Kinondoni. Sikuondoka mtupu. Leo naambiwa umeondoka kurudi kwa Muumba. Acha nikulilie Reginald A. Mengi. RIP true and valued legendary.


Maxence Mello, Mwanzilishi wa Jamii Forums.com na FikiraPevu.com ameandika kwenye ukurasa wake wa tweeter, Imekuwa asubuhi ngumu; kuamka na kupata taarifa ya kifo cha mzee wetu ambaye amekuwa na mchango mkubwa katika sekta mbalimbali hapa nchini, Dkt. @regmengi Kwa majonzi makubwa, natoa
pole kwa Familia, Wafanyakazi wa IPP, jamaa na marafiki wote kwa msiba huu
mkubwa
#RIPMengi


Diamond Platnumz kwa jina hakisi Nassib Abdul, mwanamuziki maarufu wa Bongo Flava, ameandika kwenye ukurasa wake wa Instergram, “Dah! What a Sad news....May your Humbled Soul Rest in Paradise.


Halima James Mdee, Mbunge wa Kawe, ameandika kwenye ukurasa wake wa tweeter, Nimepokea kwa Masikitiko MAKUBWA SANA kifo cha Ndugu Reginald Mengi. Nawapa POLE sana FAMILIA,JAMAA na Marafiki. Mwaka 2019 unaendelea kuwa wa MAJONZI kwetu kama TAIFA,TUNAPOTEZA watu MAKINI waliokuwa na MCHANGO mkubwa SANA katika ujenzi wa NCHI yetu.Upumzike kwa AMANI Mkuu.


Absalom Kibanda, Mwenyekiti mstaafu wa TEF. “Pumzika kwa amani Reginald Abraham Mengi. Ulinishika mkono kama mzazi, kiongozi, mshauri, mwalimu na rafiki wakati wa heri na nyakati za uhitaji. Umeacha alama ya pekee kwangu na kwa taifa zima #RIPReginaldMengi

No comments:

Post a Comment