Mtu
mmoja ajulikanaye kwa jina la Michael John Mwandu mwenye umri wa miaka
54 mkazi wa Dumila wilaya ya Kilosa amejiua mwenyewe kwa kunywa sumu
baada ya kufanya mauaji ya kumuua mke wake Leonola Ernest mwenye miaka
37 akiwa na ujauzito wa miezi kati ya 7 hadi 8.
Tukio hilo limetokea tarehe 24/5/2019 usiku huko Dumila mkoani Morogoro.
Akizungumza na waandishi wa habari Leo Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa
wa Morogoro ASCP Wilbrod Mutafungwa amewataja marehemu wengine kuwa ni
mama mkwe wa muuaji Magreth Yohana mwenye umri wa miaka 59,Salma Iddi
jirani yao mwenye umri wa miaka 52 na pamoja yeye mwenyewe marehemu
Michael John ambaye amejiua baada ya kufanya mauaji hayo.
Chanzo cha vifo hivyo ni wivu wa kimapenzi alioubaini akimtuhumu mke
wake kuwa na mahusiano na mwanaume mwingine huku akidai hao wengine
walikuwa wakifahamu jambo hilo.
Marehemu ametumia panga kumuua mama yake mkwe huku yeye na marehemu
wengine wakinywa sumu aina ya Carbon Furan ambayo ni dawa ya kuua wadudu
kwenye mimea
Baadhi ya waandishiwa habari wakimsikiliza Kamanda wa Jeshi la Polisi
mkoa wa Morogoro ASCP Wilbrod Mutafungwa wakati akizungumzia mauaji
hayo.
Baadhi ya ushahidi ulioonyeshwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro ACP Wilbrod Mutafungwa.
No comments:
Post a Comment