Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini,
Lazaro Nyalandu amekamatwa na TAKUKURU akiwa anasimamia uchaguzi wa kata
wa CHADEMA mkoani Singida.
Mkurugenzi wa Itikadi na Uenezi wa chama
hicho, John Mrema, amethibitisha tukio hilo na kusema kuwa Nyalandu
amechukuliwa akiwa kwenye kikao cha chama cha ndani.
"Nyalandu alikuwa kwenye kikao cha ndani
ili kuhamasisha uchaguzi wa ndani wa chama, na awali alichukuliwa na
polisi hivyo tumewatuma mawakili wetu tayari kufuatilia juu hilo",
amesema Mrema.
Taarifa za awali zilidai kuwa, Nyalandu
amekamatwa na kuchukuliwa na watu waliokataa kujitambulisha akiwa kwenye
kikao cha ndani cha CHADEMA kwenye kata ya Itaja, wilaya ya Singida
vijijini mkoani Singida.
Wengine waliokamatwa ni Mwenyekiti wa kata hiyo na aliyekuwa mgombea ubunge wa Chadema wa jimbo hilo, David Jumbe.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP
Sweetbert Njewike amesema taarifa hizo ni za uzushi; “Ndugu mwandishi
umefanya vyema kuniuliza, watu wanazusha uongo mitandaoni, watafuteni
TAKUKURU watawapa ukweli wa jambo hilo, polisi hawajamkamata.”
No comments:
Post a Comment