Polisi
jijini Mwanza imemkamata askari magereza Kibemba Warioba (27) mwenye
namba za usajili B.9205 WDR, akiwa na simu tano za aina tofauti na
mitandao tofauti akijihusisha na makosa ya kujipatia pesa kwa njia ya
udanganyifu.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro amesema kuwa tukio hilo
limetokea juzi saa nne na nusu asubuhi, ambapo polisi wa mkoa wa Mwanza
kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi la Mkoa wa Kagera walifanikiwa
kumkamata mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa anafanya kazi wilayani
Biharamulo mkoani Kagera na tayari amesimamishwa kazi kwa hatua zaidi za
kisheria.
Kamanda
Muliro alisema polisi walimbaini mtuhumiwa huyo akitumia njia ya
mitandao hiyo ya simu ambapo alianzisha Saccos ‘Bandia,’ iliyojulikana
kwa jina la Info Tell CCM, akilenga kuwatapeli wanachama wa CCM na
wengine katika mikoa ya Mara na Kagera.
Alitoa onyo kwa wananchi wenye tabia ya kufanya vitendo hivyo vya uhalifu waache mara moja kwa kuwa ni kinyume cha sheria.
No comments:
Post a Comment