Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi
Mkoani Arusha bwana Loata Erasto Sanare akieleza jambao baada ya
kutembelewa na Naibu Waziri Kilimo Mhe. Omari T. Mgumba katika ofisi ya
chama hicho hivi karibuni.
Naibu waziri Kilimo Mhe. Omari T.
Mgumba (Mb) akiwa ofisi ya mkuu wa mkoa wa arusha alipokutana na
wataalamu wa kilimo ,ushirika na umwagiliaji kabla ya kuanza ziara ya
kuzungukia maeneo mbalmbali mkoani hapo.
………………………….
Bashiri Salum,Wizara ya Kilimo Arusha
Vyama vya Ushirika vimeshauriwa
kukopa fedha kwenye Mabenki kwa ajili ya wanachama wao kwa kuwa
waliowengi hawakopesheki hivyo kufanya shughuli za kilimo kuwa ngumu.
Akizungumza katika kikao kilicho
wakutanisha Maafisa Ushirika, umwagiliaji na afisa kilimo Mkoani Arusha
Naibu Waziri Kilimo Mhe. Omari Mgumba amesema miundombinu mingi ya
umwagiliaji inahitaji marekebisho makubwa ili kuweza kutumiwa na
wakulima.
Aidha miundombinu hiyo imekosa
ukarabati kutokana na wakulima kutokuwa na mitaji ya kutosha na
kutoaminiwa na taasisi za fedha kusaidia ukarabati huo.
Ameshauri tume ya Ushirika
kuvisimia vyama vya ushirika ili viweze kukopa fedha Benki Kwa ajili ya
wanachama lengo likiwa ni kufanya ukarabati Wa miundombinu ya
umwagiliaji ambapo kila mwanachama atawajibika kuchangia huduma hiyo.
Hatuwezi kufanya Kilimo cha
kibiashara Kwa kutegemea mvua ambazo Nazo zimekuwa haziyabiriki
nawashauri tume ya Ushirika na tume umwagiliaji kusimamia vyama hivyo
kwenye skimu mbalimbali za umwagiliaji kukopa fedha ambazo zitatumika
kurekebisha miundombinu ya umwagiliaji badala ya kutegemea serikali
.alisema Mhe. Naibu Waziri
Naibu Waziri aliwataka maafisa
ugani kuwafikia wakulima na kuelimisha namna ya kutumia na kutoa elimu
juu ya matumizi bora ya viuatilifu vya mimea ili kupambana na visumbufu
vya mazao ambavyo vimekuwa vikimsababishia mkulima hasara kubwa.
Naye afisa Umwagiliaji wa
kanda mhandisi Juma Mdete amesema katika ukanda huo eneo ambalo linafaa
kwa kilimo cha umwagiliaji ni hekta elfu 40 kati ya hilo linalotumika ni
hekta elifu 24 tu
Amesisitiza kwamba pamoja na
matumizi kidogo ya eneo la umwagiliaji lakini maeneo yanayomwagiliwa
yanasaidia upatikanaji wa chakula wakati wa ukame.
Akichangia wakati wa mjadala huo
Afisa Kilimo Mkoa wa Arusha Bwana Daniel Loiruck amethibitisha kwamba
ukiondoa Magonjwa ya mlipuko na uvamizi wa visumbufu vya mimea maafisa
kilimo wamekuwa wakijitahidi kuwafikia wakulima ili kutatua changamoto
zinazowakabili.
Naye mwenyekiti wa chama cha
mapinduzi mkoani Arusha bwana Loata Erasto Sanare akamueleza Mhe. Naibu
waziri kwamba hali ya ukame mkoani humo ni kubwa hivyo kuishauri
serikali kuanza kufikiri njia mbadala ya kupambana na hali hiyo.
‘Msimu wa kilimo upo katikati
lakini mpaka sasa hakuna mvua na tumezunguka sehemu mbalimbali hapa
arusha mahindi yamekauka hata mvua ikinyesha haiwezi kuleta mabadiliko
tunaishauri serikali kufikiri mbinu za kukabiliana na hali hiyo’. Alisisitiza bwana Loata Sanare
No comments:
Post a Comment