NA EMMANUEL MBATILO
Taasisi ya Saratani
ya Ocean Road kushirikiana na agency inayoshughulikia maswala ya atomic
inayoitwa International atomic energy atomic wamefungua mafunzo kwa
wataalamu kujifunza namna ya kuboresha ubora wa hutoaji huduma za
mionzi.
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika mganga mkuu wa serikali
Mohammed Kambi amesema kujitokeza kwa wataalamu kutoka katika nchi za
Afrika kwenye mafunzo hayo watabadilishana mawazo na kujifunza namna ya
kuhakikisha ubora wa huduma zinazotolewa ziko vizuri.
Aidha kwa upande wa
mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Saratani Ocean Road, Julius Mwaisalege
amesema kuwa katika mafunzo hayo wanataka kuwajengea uwezo wa kutumia
njia bora na sahihi katika mashine zinazotumika katika huduma ya Nuclear
medicine.
“Ni muhimu sana
utumiaji wa hii dawa (Nuclear medicine) pamoja na uchunguzi wa hizi
mashine uweze kutolewa kwa njia sahihi sana kama unavyojua mionzi ni
mizuri katika tiba na si salama kama mtu atatumia kwa njia isiyosahihi”.
Amesema Mwaisalage.
Mafanzo hayo
yatachukua siku tano kuanzia leo Aprili 1 mpaka Aprili 5 ambapo
wataalamu kutoka sehemu mbalimbali barani Afrika wamehudhulia mafunzo
hayo
No comments:
Post a Comment