Pages

Monday, April 29, 2019

TAKA NGUMU KUBORESHWA KUWA MALI


AA
Waziri wa Mazingira Mh. January Makamba akiongea na waandishi wa habari baada ya mkutano uliofanyika ukumbi wa mkutano katika jengo la Millennium Tower jijini Dar es Salaam ambapo uliwakutanisha na wadau mbalimbali kujadili namna ya kudhibiti taka na kuwa biashara
…………………
NA EMMANUEL MBATILO
Viongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wamekutana na wadau mbalimbali wa kudhibiti taka ngumu kwa lengo la kujadili namna ambayo wanaweza kukusanya taka na kuzifanya kuwa
shughuli ya biashara na ajira.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa raisi, mazingira na muungano Mh. January Makamba amesema kuwa mfumo wa ukusanyaji taka ni muhimu hasa serikali kuweka mazingira ya kisera, kisheria na kiuchumi ili takataka ziwe mali.
“Tumeona watu wanaokusanya taka mtaani na katika majumba yetu kila siku muda mwingine tunaeaona kama vichaa kutokana na kuokota taka hizo ikiwemo makopo lakini hiyo ni shughuli ya ajira na ya kipato na tunaamini kwamba ilasimishwe”. Amesema Makamba.
Aidha Waziri huyo amesema kuwa miundombinu ya miji lazima iboreshwe hasa wao kama serikali wanajukumu la kuboresha miundombinu ikiwemo madampo, mifereji pamoja na kuweka sehemu ya kutupa na kukusanya.
“Sera, sheria, kanuni na taasisi kwamba suala la ukusanyaji wa taka na udhibiti wa taka lazima lifanywe na taasisi mahususi kwa ujumla na lazima kuwepo na sheria ikiwemo sheria ndogo na sera ambazo zitawezesha shughuli ya taka iwe biashara na ifanyike kwa urahisi.
Waziri Makamba amemalizia kwa kusema kuwa shughuli ya ukusanyaji wa taka lazima uwe shirikishi kuanzia wanaokusanya,wanaozalisha taka na viongozi pamoja na wasasi.
Kwa upande wa Naibu Makamo Mkuu wa Chuo Utafiti, Profesa Cathbert Kimambo amesema mkutano huo ambao umewashirikisha wadau wa nje na ndani watajadili na kusambaza taarifa na matokeo ya kitafiti na yakitaalamu kuhusu masuala ya ukusanyaji wa taka ngumu.
Vilevile upande wa Mratibu wa kitengo cha tafiti za sera na utetezi Chuo Kikuu Dar es Salaam shule kuu ya biashara Dkt. Goodluck Charles amesema katika tafiti ambazo zimefanyika ni kuangalia njia za kuboresha masuala ya kukusanya, kusafirisha na kuchakata taka ngumu katika jiji la Dar es Salaam na katika majiji mengine.
“Tumefanya utafiti unaohusisha teknolojia rahisi ambayo wakusanyaji taka na wengine walioko kwenye mnyonyoro wa thamani wa taka wanaweza kuzitumia ili kuboresha thamani ya taka na kuona taka ni mali “. Amesema Dkt. Charles.

No comments:

Post a Comment