Pages

Monday, April 29, 2019

FCS YAENDESHA MJADALA WA UMUHIMU WA WANAHABARI KUSHIRIKIANA NA ASASI ZA KIRAIA



 

 
Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society akiongea na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es salaam.
Mtafiti na Muwezeshaji wa semina hiyo Bw. Nick Oyoo akitoa masilisho juu ya utafiti waliyoufanya.
 Baadhi ya washiriki wakifuatilia semina kwa umakini.
Semina ikiendelea.
Katika kuendelea
kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata 
maendeleo stahiki Taasisi ya Foundation
for Civil Society (FCS) imewakutanisha wana Asasi za Kiraia(AZAKI) pamoja
na waandishi wa habari kuweza kuziangalia changamoto mbalimbali wanazokabiliana
nazo katika majukumu yao ya kazi.
Akiongea na waandishi
wa habari mapema leo katika hotel ya Double Tree Masaki jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Bw.
Francis Kiwanga amesema kuwa AZAKI na waandishi wa habari ni watu muhimu katika
jamii kwa kuwa wanafanya kazi moja ya kuhakikisha wananchi wanapata
maendeleo.
 
Aidha Bw. Kiwanga
amesema kuwa kwa sasa FCS ipo katika hatua ya mwisho ya ukaguzi (Due diligence)
wa asasi za kiraia 221 zilizopita katika mchujo wa maombi ya ruzuku za kutekeleza
miradi mbalimbali ya maendeleo, Na asasi hizo zimepita kutoka katika jumla ya
maombi 1004 yaliyopokelewa kwa mwaka huu.
 
Ameongeza kuwa
Mikoa iliyoongoza katika kutuma maombi hayo ni Dar es salaam, Mwanza, Pwani,
Morogoro na Tanga, Kwa upande wa Zanzibar mkoa ulioongoza ni wa Kusini Zanzibar,
Na mikoa iliyokuwa na muitikio mdogo imeelezwa kuwa ni Sogwe, Rukwa, Geita,
Simiyu Manyara, Katavi na Kusini Unguja.
 
Ameendelea kusema
kuwa hatua hii ni ya mwisho ya uchambuzi wa kina wa asasi zilizoomba ruzuku, na
FCS hupitia taarifa, mifumo, uadilifu na uhalali wa taasisi hizo na miradi
wanayoitaka kutekeleza, na kwa mwaka huu watatoa ruzuku kwa AZAKI 15O kutokana
na utaratibu mpya wa kufanya kazi kimkakati katika kuwezesha Asasi za Kiraia
hapa nchini.
 
Na mwisho
amemaliza kwa kusema kuwa kutokana na ushindani mkubwa kwenye maombi yaliyopelekwa,
kumekuwa na viashiria vya utapeli na udanganyifu kwa baadhi ya watu kutumia vibaya
jina la taasisi yake na zile zilizoomba ruzuku.
 
“Utaratibu
wetu upo wazi na hauna mchezo mchezo haturuhusu uvunjifu wa uadilifu wa aina
yeyote kwenye mchakato mzima wa kuomba, kukagua na kuchagua maombi yanayopata
ruzuku za FCS. Na uzuri ni kwamba tumejiwekea sera na taratibu za wazi za kutoa
taarifa kwa siri ya kuripoti matukio ya aina hii, aidha yanayohusu asasi
tunazofanya nazo kazi ama wafanyakazi na watoa huduma wa FCS” alisema Kiwanga
 
Kwa upande
wake Mtafiti na Muwezeshaji wa semina hiyo Bw. Nick Oyoo Kasera amesema kuwa majibu
ya utafiti huo yanaonyesha kuwa Waandishi wamekuwa wakizitupia lawama AZAKI, kwa
kusema wengi wamekuwa wakifanya kazi bila kuwa na tafiti wala takwimu, na wengi wao wamekuwa wakifanya kazi kwa matukio wakiona maadhimisho yanakaribia ndipo
wanaanza kutafuta taarifa.
 
Ameongeza kuwa
kwa upande wa AZAKI nyingi zimekuwa zikitoa lawama kwa wanahabari kudai posho
ili kutoa taarifa zao jambo ambalo limekuwa likizinyima haki taasisi ndogo
ndogo kuweza kufikisha ujumbe kwa wanajamii.
 
Na mwisho
amewasihi Wahariri kuweza kuweza kutoa fursa kwa stori za taasisi zinazofanya kazi za kijamii na kuondokana
na mawazo mgando ya kuwa waandishi wao wamechukua posho katika kazi hizo, na amewaomba viongozi wa taasisi hizo kuwa baada ya kupata ruzuku huwa maisha yao
yanabadilika na kuwa na matanuzi makubwa hali inayosababisha waandishi wa habari kuwaelewa vibaya.

No comments:

Post a Comment