Pages

Tuesday, April 30, 2019

LUGOLA ASHTUKIZA KITUO CHA POLISI STAKISHARI JIJINI DAR ES SALAAM, ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI WALIOFIKA KITUONI HAPO, AWAHOJI MAHABUSU MMOJA BAADA YA MWINGINE


PIX 1A
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akiingia Kituo cha Polisi Stakishari, jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kushtukiza katika Kituo hicho kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wa Jeshi la Polisi nchini. Pia Lugola aliwahoji wananchi waliofika kuwachukulia dhamana ndugu zao waliopo ndani ya kituo hicho, pamoja na mahabusu wote  waliopo kituoni hapo.
PIX 2A
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akiwahoji wananchi mbalimbali katika mapokezi ya Kituo cha Polisi cha Stakishari, jijini Dar es Salaam, leo, walipofika kituoni hapo kwa ajili ya kuwachukulia dhamana pamoja na kupata huduma zinginezo kituoni hapo. Pia Lugola aliwahoji wananchi waliofika kuwachukulia dhamana ndugu zao waliopo ndani ya kituo hicho, pamoja na kuwahoji mahabusu wote  waliopo kituoni hapo.
PIX 3A
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Kipolisi Ukonga, jijini Dar es Salaam, Frank Duma, alipokua anatoa taarifa ya utendaji kazi ya Wilaya hiyo. Waziri huyo alifanya ziara ya kushtukiza katika Kituo cha Polisi cha Stakishari yenye lengo la kufuatilia utendaji kazi katika kituoni hapo.  Pia Lugola aliwahoji wananchi waliofika kuwachukulia dhamana ndugu zao waliopo ndani ya kituo hicho, pamoja na kuwahoji mahabusu wote waliopo kituoni hapo.
PIX 4A
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akiongozana na viongozi wa Kituo cha Polisi cha Stakishari, jijini Dar es Salaam, wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho, leo. Lugola aliwahoji wananchi waliofika kuwachukulia dhamana ndugu zao waliopo ndani ya kituo hicho, pamoja na mahabusu wote waliopo kituoni hapo.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
…………………..
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amefanya ziara ya kushtukiza Kituo cha Polisi Stakishari jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufuatilia utendaji kazi wa Kituo hicho.
Waziri Lugola aliwasili kituoni hapo Saa 6:16 mchana ambapo alikutana na
wananchi mapokezi ya kituo hicho ambao walifika kwa ajili ya kuwachukulia dhamana ndugu zao walipo katika mahabusu ya kituo hicho, aliwahoji kama wanapata huduma nzuri kutoka kwa askari wa kituo hicho.  
Pia Waziri Lugola akiwa katika mapokezi ya kituo hicho, alikichukua kitabu cha taarifa za watuhumiwa wote waliopo mahabusu na baadaye kuelekea katika mahabusu hiyo akiwahoji watuhumiwa wote kwa kuwaita kwa majina kujua makosa yao yaliyoyafanya wawepo kituoni hapo.
Akizungumza mara baada ya kumaliza kuiwahoji mahabusu hao, alisema ziara yake ni ya kawaida ya kufuatilia utendaji kazi wa vituo vya polisi, pia kufuatilia ahadi zake ambazo alizitoa Bungeni kufuatilia vituo mbalimbali vinavyolalamikiwa, na pia yeye Waziri ni wajibu wake kufuatilia utendaji kazi pamoja na maagizo anayoyatoa mara kwa mara ya dhamana zitolewe saa 24 ikiwemo Jumamosi na Jumapili na pamoja na polisi kutowabambikizia kesi wananchi.
“Lengo la hii ziara yangu ni kuboresha utendaji kazi wa vituo vya polisi nchini, sijaja kumuadhibu mtu mimi, hivyo msiwe na wasiwasi, bali kilichonifanya hapa nije nikufuatilia maagizo mbalimbali ambayo niliyatoa kama kweli mnayafanyia kazi,” alisema Lugola.
Lugola aliwataka Makamanda wa polisi mikoa mbalimbali nchini, kusimamia utendaji kazi bora na kuakikisha maagizo yake anayoyatoa yanafanyiwa kazi ipasavyo, na ataendelea kuyafuatilia maagizo yote anayoyatoa na endapo yakipuuzwa hatamvumilia mtu.

No comments:

Post a Comment