Na
Christian Gaya
Kampuni za bima zinahitaji kuwa na uaminifu wa
hali ya juu ili kupata kupata wateja wengi na hatimaye kukuza sekta ya biashara
ya bima nchini. Bima ni kitu cha muhimu sana kwa ajili ya kujenga amani ya
moyo, kuleta hifadhi na kulinda watu na mali zao kutokuwa na wasiwasi wowote
juu ya kitu chochote kinapopatwa na janga lolote. Bima inamfanya mtu kujengeka
kimapato kwa ajili ya ...
kupata mahitaji muhimu kwa siku zijazo.
Wanabima mara nyingi wao wanauza ahadi, na
uaminifu ni kitu cha umuhimu sana kwa mtoa au muuzaji wa bima yeyote kuliko
biashara ya aina nyingine yeyote ile. Mkataba ndio unaosema ukweli juu ya madai
yanayotakiwa aliyekatiwa bima kisheria alipwe kwa kubadilishana na tozo ya bima
iliyofanyika katika mkataba huo.
Mtoa bima anaahidi kulipa hasara
itakayosababishwa na janga ambalo limo ndani ya mkataba. Ahadi ni kama
kiashirio fulani, ambacho kilikuwa hakileti mantiki sana. Hii ina maana ya
kwamba pale unaposhidwa kutimiza ahadi ya mwanzo, wasiwasi ndipo unapoanza
kupanda katika akili za watu juu ya
hicho mtu kilichomjia akilini mwake. Kwa hiyo uaminifu ni jiwe la msingi mkubwa
kwa biashara yeyote ile.
Kwa bahati mbaya changamoto kubwa ambayo sekta ya
bima nchini hapa inayo ni hii ya kuwa na uaminifu mdogo kutoka kwa wananchi wa
Tanzania. Wakati mwingine inatokea juu
ya tofauti ya maoni mbalimbali yanayoohusiana na tafsiri za taratibu na sheria
za vifungu vya bima yenyewe kati ya kampuni ya bima na mnunuzi wa huduma au bidhaa
za bima na mara nyingi hutokea mpaka kushtakiana kati yao.
Mashtaki mengi yanatokea hasa wakati wa madai
yanapofanyika. Mara nyingi wateja wanakuwa hawana mahali ambapo wanaweza
kupeleka malalamiko na dukuduku zao. Kinachotokea ni kukata tamaa kabisa na
kuamua kutokata bima ya aina yeyote tena. Na baadhi ya uzoefu mbaya unaotokea
unaanza kusambaa kwenye familia na marafiki na hatimaye sekta ya bima kukosa
uaminifu miongoni mwa watanzania wengi.
Ijulikane wazi ya kuwa watu wengi miongoni mwa
watanzania hawajui ya kuwa kamishana wa bima ambaye ndiye msimamizi wa sekta
hii ya bima na kwamba matatizo kama hayo yanaweza kupelekwa na kutatuliwa na
kamishana hii yaani TIRA. Na hata wachache wanaopeleka malalamiko yao ili
yatatuliwe bado wanakosa uaminifu na sekta hii na hata baada ya malalamiko yao
kutatuliwa, kwa kuamini ya kuwa asingekuwa kamishna wangepoteza haki zao. Na
tabia hii mara nyingi inasababisha wasikatie majanga hatarishi tena.
Hivyo, swali kubwa hapa ni, jinsi gani wauza bima
wataweza kufikia kujenga na kupandisha uaminifu ndani ya soko hili ambalo liko
wazi kabisa na la kutamanisha? Kwa sababu ni wauza bima wenyewe wanaoweza
kurudisha uaminifu tena kwa wananchi kwa sababu wao ndio waliokuwa wameupoteza.
Kupatikana kwa uaminifu kutoka kwa umma
kunahitaji kuweka wazi sifa za bidhaa, na kuwa wa ukweli na uwazi juu ya
sheria, vipengele na taratibu zote na hasa kuanzia mwanzo pale kabla ya kuuziwa
au wakati anapouziwa bima. Tunataka mteja aweze kungundua kipengere chochote
atakachooona ya kuwa hakimfai mapema kabisa.
Kutoa habari zisizokamilika ili kumshawishi mteja
anunue bima ni jambo ambalo halikubaliki hata kidogo kisheria na hapo ndipo
uaminifu unapo potea kabisa na hata madai hayawezi kutambulika. Kumbuka ya kuwa
thamani kubwa ya biashara ya bima ni usimamizi wa madai. Kama madai hayawezi
kusimamiwa vizuri, uaminifu ndipo hapa hupotea moja kwa moja.
Jambo la pili, faida kubwa ya uaminifu inakuwa
ndani ya mteja mwenyewe ambayo baadaye inaweza kujenga uhusiano wa muda mrefu n
ahata kwa njia ya maneno ya mdomoni. Uaminifu katika biashara ya bima ni ya
muhimu sana kwa muuza bima kuliko aina yeyote ya biashara, sababu kubwa ni
kwamba kwenye bima kinachouzwa ni ahadi.
Huduma bora kwa mteja inatakiwa kutolewa hata
baada ya kuuza bima/kuingia au kusaini mkataba na hasa huduma bora kwa mteja
inahitaji pale madai ya bima yanapofanyika au yanapofunguliwa.
Huduma bora kwa mteja ni njia ya nyingine ya
muafaka ya kujenga na kuendeleza uaminifu. Sekta ya bima inahitaji kuboresha
usimamizi wa uhusiano wa mteja wa muda mrefu, kwa mfano ukichukulia faida ya
kutumia njia ya digitali katika kutoa huduma bora. Uzoefu huu wa teknolojia ya
habari na mawasiliano inawapa wateja na watu wengine moyo wa kujaribu kufanya
mahusiano magumu ya bima kwa njia ya mtandao.
Kuwa na mazungumzo na mshauri wa masuala ya bima
kwa kuongea kwa njia ya vidio juu ya jinsi ya kufungua madai inamsaidia mteja
vizuri zaidi kufahamu habari waliyobadilishana, na maulizo mengi ya bima
yanaweza kumalizwa kwa njia rahisi kama vile ya mazungumzo ya kwa njia ya WhatsApp.
Kama sekta ya bima inahitajika kuliangalia jambo
hili kama wana bima mlichokifanya ili kumtimizia mahitaji yenu na mahitaji ya
wateja wenu. Leo wateja mara nyingi wanaangalia njia bora na rahisi ya kufanya
biashara. Wana bima mnahitaji kuendelea kujikumbusha nyie wenyewe juu ya
mabadiliko ya mpito wa soko la bima, ya kwamba haiwekani kwa sasa kutegemea
utamaduni au mfumo wa kienyeji wa jinsi ya kufanya biashara and njia za
usambazaji. Mnahitaji hasa zaidi, kuwekeza kwenye ubunifu, utafiti na
kujiendeleza kwenye mbinu za uuzaji ili kutoa uaminifu unaotakiwa na kuhakikisha
ya kuwa biashara inakua.
No comments:
Post a Comment