Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimia wananchi
waliokuja kumlaki wakati akiwasili kwenye mgodi wa Almasi Mwadui mkoani
Shinyanga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
………………………………………………………………………………..
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 28 Februari,
2019 amefanya ziara ya kikazi katika wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga
ambapo ametembelea mgodi wa Almasi wa Mwadui (Williamson Diamond Ltd) na
kujionea shughuli za uchimbaji wa almasi pamoja na kupokea taarifa ya
mgodi huo.
Aidha alitembelea Shule ya
Sekondari Shinyanga na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa maabara, kuona
mashine ya uchapaji wa maneno maalum kwa wasioona na kuzungumza na
wanafunzi wa shule hiyo.
Akizungumza na Wanafunzi wa
Shule hiyo Makamu wa Rais amesema ziara yake hapo ilikuwa ya kuja
kuwasalimu na kuona na kutambua changamoto zinazowakabili na kuwaahidi
Serikali itazitatua na kuwataka wanafunzi hao kusoma kwa bidi na
kuwataka walimu na wanafunzi wa kawaida kutowabagua au kuwaambia maneno
ya maudhi wenzao wenye ulemavu.
Makamu wa Rais ambaye
ameongozana na Manaibu Waziri kutoka Wizara za Madini, TAMISEMI, Maji,
Ujenzi, Kilimo na Ardhi kwa pamoja walitembelea mradi wa kituo cha Afya
Kishapu ambao umekamilika kwa zaidi ya asilimia 95% na umejengwa kwa
fedha za Serikali shilingi milioni 400.
Akihutubia kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyika Mhunze, Makamu wa Rais amewapongeza wananchi wa
wilaya ya Kishapu kwa kushiriki kwenye shughuli za maendeleo ambapo pia
mkoa unauhakika wa tani zaidi ya laki tano na ishirini elfu.
Makamu wa Rais pia amekemea
vitendo vya rushwa mkoani Shinyanga kwani kesi nyingi za mimba za
utotoni zimeshindwa kuchukuliwa hatua stahiki za kisheria kutokana na
rushwa kutawala.
Kwa upande wa Bima ya Afya,
Makamu wa Rais ameukumbusha Uongozi wa mkoa huo na wilaya zake kuongeza
juhudi za kuhamasisha wananchi kuwa na bima ya afya.
“Kati ya Kaya 40,000 ni kaya 4000 tu zimechukua bima ya afya hapa Kishapu” alisema Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimia wanafunzi
waliokuja kumlaki wakati akiwasili kwenye mgodi wa Almasi Mwadui mkoani
Shinyanga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Meneja wa Huduma za Kiufundi wa
Mgodi wa Williamson Diamond Richard Jumanne akimuonyesha Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan eneo ambalo
uchimbaji wa almasi unafanyika katika mgodi huo uliopo Mwadui,
Shinyanga. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akiangalia shughuli ya uchambuaji
wa almasi klatika mgodi wa Wiliamson Diamond Ltd, wengine pichani ni
Naibu Waziri Madini Mhe. Stanslaus Nyongo (kushoto) na Naibu Waziri wa
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelline Mabula pamoja na
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Mwita Waitara (kulia).
Makamu wa Rais yupo mkoani Shinyanga kwa ziara ya kikazi. (Picha na
Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi wa
ujenzi wa maabara ya shule ya Sekondari Shinyanga. (Picha na Ofisi ya
Makamu wa Rais)
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Shinyanga mara baada
ya kuweka jiwe la msingi wa ujenzi wa maabara . (Picha na Ofisi ya
Makamu wa Rais)
Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya
Sekondari Shinyanga wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye yup kwenye ziara ya kikazi
mkoani humo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi wa
Kishapu kwenye uwanja wa mikutano Mhunze mkoani Shinyanga. (Picha na
Ofisi ya Makamu wa Rais)
No comments:
Post a Comment