Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Tigo Tanzania Simon Karikari (wa pili kulia) akikata utepe kuashiria
kumkabidhi rasmi nyumba mzee Joram Mollel (93) ambaye amekuwa akishiriki
mbio za Tigo Kili Half Marathon kwa miaka minne mfululizo. Kulia kwake
ni mzee Mollell akifautiwa na mwanaye Elibarik Mollel pamoja na Afisa
Biashara Mkuu wa Tigo Tarik Boudiaf. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa
wiki katika eneo la Mushono jijini Arusha. Kulia ni kaimu Mkurugenzi wa
Tigo Kanda ya Kaskazini, Aidan Komba
Babu Joram Molle (93) akitoa
neno la shukrani muda mfupi baada ya kukabidhiwa nyumba na Kampuni ya
Tigo kutokana na ushiriki wake wa mbio za Tigo Kili Half Marathon kwa
miaka minne mfululizo. Wanaomsikiliza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Tigo Simon Karikari akifuatiwa na Afisa Biashara Mkuu Tarik Boudiaf, na
kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini Aidan Komba. Hafla
hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika eneo la Mushono jijini Arusha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Tigo Tanzania Simon Karikari, akimkabidhi fungua za nyumba mzee Joram
Mollel ikiwa ni kama zawadi na kukubali mchango wake kwa mbio za Tigo
Kili Half Marathon kwa miaka minne mfululizo pamoja na umri mkubwa.
Anayeshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini Aidan
Komba. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika eneo la Mushono
jijini Arusha.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni
ya Tigo Tanzania wakiwa katika picha ya Pamoja muda mfupi baada ya
Kampuni hiyo kumzawadia nyumba mzee Joram Mollel mkazi wa Jijini Arusha
ikiwa ni kutambua mchango wake katika mbio za Tigo Kili Half Marathon
ambazo mzuee huyo ameshiriki kwa miaka minne mfululizo. Hafla hiyo
ilifanyika mwishoni mwa wiki katika eneo la Mushono jijini Arusha.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni
ya Tigo Simon Karikari akizungumza na wahabari hawapo pichani wakati wa
hafla ya kumkabidhi nyumba Mzee Joram Mollel (93), aliyekuwa akikimbia
mbio za Tigo Kili Half Marathoni kwa miaka minne mfululizo, kulia ni
Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini Aidan Komba. Hafla hiyo
ilifanyika mwishoni mwa wiki katika eneo la Mushono jijini Arusha.
………………………..
Na Mwandishi Wetu, Arusha
KAMPUNI ya Mawasiliano ya Tigo
imemkabidhi nyumba ya vyumba 17 ikiwa na samani zote za ndani Babu Joram
Mollel (93), kutokana na ushiriki wake wenye mafanikio katika mbio za
Tigo Kili Half Marathon kwa miaka mine mfululizo.
Hafla ya makabidhiano hayo
ilifanyika eneo la Mushono nje kidogo ya Jiji la Arusha, ikiongozwa na
Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo Simon Karikari pamona na Afisa Biashara mkuu
Tarik Boudiaf
Akizungumza kwenye hafla hiyo
Karikari alisema, nyumba hiyo ilinunuliwa na kukarabatiwa kisha
kumkabidhi Babu Mollel kama ishara ya shukrani kwa kujituma na umahiri
wake katika riadha.
‘Babu Mollel amekuwa
akishiriki mashindano ya Tigo Kili Half Marathoni kwa miaka mingi sasa.
Tulipoona hali ya makazi yake si nzuri Tigo tuliona njia sahihi ni
kuwezesha apate nyumba yake mwenyewe,”alisema Karikari.
“Katika nyumba yake hii ya hapa
Mushono, Babu atakuwa anakaa katika nyumba ya kisasa, iliyo tayari na
samani pamoja na vyombo vyote muhimu vya ndani. Nyumba hii pia
imeunganishwa na umeme na maji. Hati ya nyumba pia ipo kwa jina lake,
hivyo yeye ndiye mmiliki halali wa nyumba hii,” aliongeza Karikari.
Aidan Komba, ambaye ni Kaimu
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini alisema kwamba nyumba imegawanyika
sehemu tatu na kuongeza kuwa Babu Mollel atakaa katika nyumba moja na
mbili zilizobaki ataweza kuzipangisha na kujipatia kipato cha kuendeshea
maisha yake ya kila siku.
“Napenda kuwashukuru sana Tigo kwa
zawadi hii ya kipekee. Maneno yangu hayawezi kuelezea furaha
niliyonayo. Ktendo hiki kina maana kubwa sana kwangu. Maana hivi sasa
ninaweza nikasema sasa nina mahali pakuita kwangu,” alisema Babu Mollel.
Ushiriki wa Babu Mollel katika
mashindano ya Kilimarathon ni wa zaidi ya miaka 15, ambapo amekuwa
akiwavutia watu wengi kumshangilia wakati akishiriki mbio za marathon,
pamoja na uzee wake. Katika miaka minne mfululizo iliyopita, Tigo
imekuwa mlezi na mdhamini mkuu wa mbio za kilometa 21 zinayojulikana
kama ‘Tigo Kili Half-Marathon’, ambayo ni nusu ya mbio kamili ya
kilometa 42 za marathon ambayo hufanyika katika vilima vya Mlima
Kilimanjaro, mlima mrefu kuliko wote barani Afrika.
“Babu Mollel ni taswira halisi ya
uanamichezo, ujasiri na jitihada. Yeye ni mfano aliye hai kwamba kama
binadamu tunaweza tukafanikiwa katika lolote lile ambacho tukiamua
kukifanya kwa dhati, na kuondoa dhana nzima kwamba umri au changamoto
zingine zozote zinaweza zikawa sababu ya kutokufanikiwa kwetu. Leo,
tunamsheherekea yeye,” alieleza Karikari kuhusu mzee huyo wa miaka 93.
Mwaka jana, Tigo ilishirikiana na
Babu Mollel katika kampeni maalum ya Tigo Kili Half-Marathon iliyoitwa
‘Tisha kama Babu’. Kampeni hiyo ilikuwa na lengo kubwa la kuhamasisha
Watanzania kuweza kuishi maisha ya kujali afya zao. Wakati huo huo, Tigo
pia ilisitisha rasmi namba ya mbio aliyokuwa akiitumia Babu Mollel
‘1040’ na alitambuliwa rasmi kama mwanamichezo wa heshima ‘Hall of
Fame’..
No comments:
Post a Comment