Mkuu wa Mkoa Kagera, Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti na baadhi ya wanakamati wa maandalizi ya mazishi ya Ruge Mutahaba mkoani Kagera.
Na Mwandishi wa Fullshangwe Bukoba
Mkuu wa Mkoa Kagera, Brigedia
Jenerali Marco E. Gaguti amesema. Mwili wa Marehemu Ruge Mutahaba
unatarajiwa kuagwa Katika viwanja vya Gyhmkana ndani ya Manispaa ya
Bukoba Kabla ya kupelekwa Kabale Halmashauri ya Wilaya Bukoba, kwa ajili
ya Ibada na Mazishi hii ni kutokana na Wingi wa watu na sehemu ya
Nyumbani kuwa Finyu.
Aidha kwa upande mwingine Mh.
Gaguti amewaomba wananchi kujitokeza kuulaki mwili wa Marehemu Ruge
popote pale utakapopita kwa ajili ya kutoa salaam za mwisho ikiwa ni
Ishara ya kumuenzi na kumuaga Mzalendo na mwanaharakati wa kweli
Marehemu Ruge Mutahaba
No comments:
Post a Comment