Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara
Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akiongea na viongozi wa Vyuo vya
Maendeleo ya Jamii pamoja na Wakurugenzi wa Wizara wakati wa kufunga
mafunzo ya siku tatu ya sheria ya manunuzi.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo
ya Jamii ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya manunuzi ya Wizara ya
Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akiongea jambo
wakati wa kuhitimisha mafunzo ya siku tatu kwa viongozi wa wizara na
Wakuu Vyuo vya Maendeleo ya Jamii jana Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Manunuzi ya Wizara ya
Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Martha Chuma akiongea jambo wakati
wa kuhitimisha mafunzo ya siku tatu kwa viongozi wa wizara na Wakuu
Vyuo vya Maendeleo ya Jamii jana Jijini Dodoma.
Baadhi ya Wakuu wa Vyuo vya
Maendeleo ya Jamii pamoja na Wakurugenzi wa Wizara ya Afya Idara Kuu
Maendeleo ya Jamii wakifuatilia jambo wakati wa kuhitimisha mafunzo ya
siku tatu kwa viongozi wa wizara na Wakuu Vyuo vya Maendeleo ya Jamii
jana Jijini Dodoma.
…………………..
Na Mwandishi wetu – Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara
Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amewaonya viongozi na baadhi ya
watumishi wa Wizara yake kuwa hakuna nafasi tena ya kufanya makosa
katika utendaji kazi kwa kuwa tayari wana ufahamu mkubwa wa sheria ya
manunuzi.
Alisema hayo wakati hotuba yake
kwa watumishi hao wakati wa kufunga mafunzo ya siku tatu kuhusu sheria
ya manunuzi nakuongeza kuwa wanatakiwa kusoma zaidi sheria hiyo baada ya
kuwa wamepata mwanga wa kutosha kutokana na mafunzo hayo.
Aidha Kiongozi huyo aliongeza kuwa
kutokana na kukosa ufahamu wa sheria ya manunuzi baadhi ya watumishi
walikuwa wanafanya makosa ya kimajukumu kwa kutekeleza majukumu ya watu
wengine na kuonya kuwa inabidi wajilizishe na sheria ili kuepuka
mwingiliano katika majukumu yao.
‘’Baada ya kupitia mafunzo ya
majukumu ya kila mtu kisheria ni matumaini yangu kuwa hakutakuwa nafasi
tena ya kufanya makosa kwa kufanya maamuzi yanayokiuka sheria na
kujikuta unatekeleza majukumu ya mtu mwingine kama vile kutekeleza
majukumu ya Katibu Mkuu wakati wewe huna mamulaka hayo.’’ Aliongeza Dkt.
Jingu.
Aidha amewataka viongozi na
watumishi hao kuepuka na makosa ya rushwa akionya kuwa makosa hayo ni
makubwa na yanashughulikiwa na vyombo husika akiwataka kujiepusha nayo
kwani mtu akibainika atapata misukomisuko mikubwa jambo ambalo
linaepukika.
Aidha amechukua fursa hiyo
kuwataka wafanyakazi wote kuacha kufanya kwa mazoea na kuwataka kuwa
wabunifu katika maweneo yao ya kazi na katika Jamii zinazowazunguka ili
jamii husika iweze kufaidika na kuwepo kwa taasisi mahali hapo.
Amewaagiza Wakuu wa Vyuo vya
Maendeleo ya Jamii kuhakikisha wanakuwa na ubunifu na pia kutumia
rasilimali zilizopo katika maeneo yanayozunguka vyuo ili wananchi
wanaoishi jilani na vyuo hivyo waweze kunufaika na uwepo wa chuo katika
maeneo yao.
‘’Kuweni wabunifu achana na
kufanya kazi kwa mazoea ili wanajamii wanao wazunguka waweze kunufaika
na uwepo wa chuo katika maeneo yao mfano Chuo cha Rundenga kwasasa
kinasindika zao la karoti na bidhaa zitokanazo na uwekezaji huo zinauzwa
kwa jamii jambo hili ni zuri sana.’’ Aliongeza Dkt. Jingu.
Mafunzo hayo kwa viongozi wa
Wizara, Viongozi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii pamoja na maafisa wa
serikali yanahusu sheria ya Manunuzi ya Serikari ya Mwaka 2011 na
mabadiliko ya kanuni zake ya mwaka 2013 kama ilivyorekebishwa mwaka
2016.
No comments:
Post a Comment