Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),
Mhandisi Joseph Nyamhanga,akizungumza wakati wa kupokea mashine 270 za
kieletroniki za ukusanyaji wa mapato (POS) zilizotolewa kwa ajili ya
halmashauri 18 za mikoa ya Dodoma na Kigoma kupitia mradi wa Kuboresha
Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (LIC) unatekelezwa kwa ushirikiano
baina ya ofisi ya TAMISEMI na Ubalozi wa Dernmark.
Kiongozi wa Mradi Maboresho ya
Mazingira ya Biashar Flemming Olsen,akitoa taarifa baada ya kukabidhi
mashine 270 za kieletroniki za ukusanyaji wa mapato (POS) zilizotolewa
kwa ajili ya halmashauri 18 za mikoa ya Dodoma na Kigoma kupitia mradi
wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (LIC) unatekelezwa kwa
ushirikiano baina ya ofisi ya TAMISEMI na Ubalozi wa Dernmark.
Baadhi ya Makatibu Tawala wa Mikoa
waliohudhuria hafla ya upokeaji wa mashine za Kielektronic POS 270
kutoka kwa Serikali ya Dernmark
Mkurugenzi wa TEHAMA OR-TAMISEMI
Erick Kitali,akitoa wito kwa halmashauri zilizokabidhiwa Mashine za
Kielektronic POS 270 kwa ushirikiano baina ya ofisi ya TAMISEMI na
Ubalozi wa Dernmark.
Kiongozi wa Mradi Maboresho ya
Mazingira ya Biashar Bw.Flemming Olsen,(kulia) akimkabidhi Mashine Ya
Kielektronic POS kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhandisi Joseph Nyamhanga
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhandisi Joseph
Nyamhanga akionesha juu mashine ya Kielektronic POS kwa makatibu Tawala
wa mikoa (hawapo pichani) baada ya kupokea mashine 270 zilizotolewa na
ubalozi wa Dernmark kwa kushirikiana na Ofisi ya TAMISEMI kulia kwake ni
Kiongozi wa Mradi Maboresho ya Mazingira ya Biashar Bw.Flemming Olsen
Kiongozi
wa Mradi Maboresho ya Mazingira ya Biashar Bw.Flemming Olsen
akimkabidhi mashine za Kieletronic Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma
Bw.Rashid Mchatta (katikati) ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhandisi Joseph Nyamhanga
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhandisi Joseph
Nyamhanga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi mara baada
ya kupokea mashine za Kieletronic POS 270 zilizotolewa na Ubalozi wa
Dernmark kwa kushirikiana na Ofisi ya Tamisemi
Katibu
Tawala Mkoa wa Kigoma Bw.Rashid Mchatta akitoa neno la shukran kwa
niaba ya wenzake baada ya kukabidhiwa mashine 270 za Kieletronic POS
zilizotolewa na Ubalozi wa Dernmark kwa kushirikiana na Ofisi ya
Tamisemi.
Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog
…………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),
Mhandisi Joseph Nyamhanga amezielekeza mamaka za serikali za mitaa kote
nchini kuhakikisha kuwa fedha zote zinazokushwanywa zinawekwa benki
kabla ya kupangiwa matumizi.
Mhandisi
Nyamhanga alitoa marufuku hiyo wakati wa kupokea mashine 270 za
kieletroniki za
ukusanyaji wa mapato (POS) zilizotolewa kwa ajili ya
halmashauri 18 za mikoa ya Dodoma na Kigoma kupitia mradi wa Kuboresha
Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (LIC) unatekelezwa kwa ushirikiano
baina ya ofisi ya TAMISEMI na Ubalozi wa Dernmark.
Mhandisi
amesema kuwa wakurugenzi wa halmashauri kote nchini wanatakiwa
kuhakikisha fedha zote zinazokusanywa zinakwenda benki kabla ya kupangia
matumizi.
“Makatibu Tawala wa Mikoa kuweni
makini katika ukusanyaji wa mapato ili kutimiza azma ya serikali ya
kuongeza udhibiti na kuleta tija katika ukusanyaji wa mapato katika
Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kuhakikisha fedha ilokusanywa
inahifadhiwa benki kabla ya matumizi yoyote”Amesema Mhandisi Nyamhanga.
Aidha Mhandisi Nyamhanga ameongeza
kuwa jitihada hizi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano zitasaidia
kuongeza kipato katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na kupunguza
utegemezi na kuboresha utoaji wa huduma za kijamii kwa watanzania wote.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
TEHAMA OR-TAMISEMI Erick Kitali ametoa wito kwa halmashauri kuwa na
kifaa maalumu cha kuzuia radi ili kutatua changamoto ya mitandao ya
mifumo ya mapato kaharibiwa radi kipindi cha mvua katika halmashauri
hizo.
Naye
Mkurugenzi wa Serikali za Mitaa, Dk Charles Mhina amesema kuwa mradi
wa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji katika halmashauri za
mikoa ya Dodoma na Kigoma, umefadhiri miradi mbalimbali yenye thamani ya
zaidi ya Sh bilioni 11.013.
Akifafanua
baadhi ya miradi iliyotekelezwa kupitia mradi huo, Dk Mhina amesema
kuwa wameweza kununua POS 235 kwa thamani ya zaidi ya Sh bilioni 1.95,
ambazo zimechangia ongezeko la makusanyo kwenye halmashauri za Mkoa wa
Kigoma kwa asilimia 88 katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Desemba
2018 na kwa asilimia 130 kwa Mkoa wa Dodoma.
Aidha
amesema kuwa pia umewezesha kujengwa kwa vituo 13 vya utoaji huduma za
biashara na uwekezaji kwa gharama ya zaidi ya Sh bilioni 1.45 ambavyo
vimepunguza urasimu wa utoaji wa huduma za biashara na uwekezaji na
kuongeza idadi za biashara na mapato ya halmashauri.
Naye Kiongozi wa Mradi Maboresho
ya Mazingira ya Biashar Flemming Olsen ametoa wito kwa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano waTanzania kuhakikisha mapato yanakusanywa kwa
ufasaha kwani kuna wafanya biashara wanabidhaa ya thamani kubwa lakini
wanalipa ushuru mdogo.
Wakati huo huo Katibu Tawala wa
Mkoa wa Kigoma Rashid Mchatta amesema kuwa atakwenda kusimamia vyema
mashine hizo ili zifanye kazi ipasavyo na itasaidia kuongeza mapato
katika maeneo yao ya kazi.
Katika hafla hiyo Mhandisi
Nyamhanga amehitimisha kwa kutoa shukurni za dhati kwa niaba ya
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa wananchi wa Serikali ya
Denmark kupitia Ubalozi wa Denmark nchini Tanzania na kusema kuwa
ushirikiano wa nchi hizi mbili utaleta maendeleo kwa wananchi wa
Tanzania kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment