Waziri wa Kilimo na Chakula Mh.
Japhet Hasunga akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya
Protea Courtyard jijini Dar es salaam kuhusu kongamano la Kilimona
Biashara linalotarajiwa kufanyika Machi 20-22 jijini Dar es Salaam
kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere kushoto ni Majabi Emmanuel kutoka
Taasisi ya (Youth Agro Summit International).
Waziri wa Kilimo na Chakula Mh.
Japhet Hasunga akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa
habari kwenye hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es salaam kuhusu
kongamano la Kilimona Biashara linalotarajiwa kufanyika Machi 20-22
jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere katikati ni
Majabi Emmanuel kutoka Taasisi ya (Youth Agro Summit International) na
kushoto ni Justin KisaiJustin Kisai Mjumbe wa Kongamano hilo na mkulima
wa Mananasi na mbogamboga kutoka Kiwangwa Chalinze mkoani Pwani
Waziri wa Kilimo na Chakula Mh.
Japhet Hasunga akifafanua jambo kuhusu kongamano la Kilimona Biashara
linalotarajiwa kufanyika Machi 20-22 jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi
wa Mwalimu Nyerere kushoto ni Majabi Emmanuel kutoka Taasisi ya (Youth
Agro Summit International) na kulia ni Neema Temba Mkurugenzi wa Sera
TPSF.
Waziri wa Kilimo na Chakula Mh.
Japhet Hasunga akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kongamano hilo
mara baada ya kumalizika kwa mkutano na waandishi wa habari.
…………………………………………………………………………………………
Asilimia 60 ya wanafunzi
wanaohitimu vyuo vikuu wanakuwa sio wazalishaji kutokana na kusubiri
ajira mbalimbali katika Serikali, Mashirika na taasisi mbalimbali huku
wakiacha kilimo ambacho ndiyo chenye ajira kubwa na ya moja kwa moja
huku wakiacha Kilimo Biashara ambacho ndiyo suluhisho la ajira kwa
vijana nchini.
Hayo ameyasema Waziri wa Kilimo
Mh. Japhet Hasunga wakati wa mkutano na waandishi wa
habari kuhusiana
na Kongamano la vijana Kimataifa kuhusu Kilimo Biashara (Youth Agro
Summit International) litakalofanyika Machi 20 hadi 22 katika ukumbi wa
Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Serikali imesema
kuwa katika kuelekea uchumi wa viwanda tunahitajika kuwekeza nguvu kwa
vijana kuingia katika Sekta ya Kilimo na kuacha kuzunguka na bahasha ya
kaki ya kuomba ajira sehemu mbalimbali katika mashirika na taasisi
nchini.
“Vijana wakiingia
katika Kilimo suala la kutembea na bahasha kwa ajili ya kutafuta ajira
litakuwa historia kwani kijana kuendesha Kilimo hakuhitaji watu wa
kufanya usaili”amesema Hasunga.
Hasunga amesema kuwa
serikali imedhamiria kuweka mazingira ya Kilimo kwenda kisasa kwa
kuhakikisha masoko ndani yanakuwa nafasi na ziada kuuza nje ya nchi.
Aidha amesema Kilimo
kimekuewa kikilimwa kwa mazoea na kufanya kilimo kuonekana kigumu
lakini serikali ya awamu ya tano tunakwenda na Kilimo cha kisasa kwa
kuhusianisha masoko pamoja na viwanda kwa kwa ajili ya kuongeza thamani
ya mazao.
Hasunga amesema nchi
yeyote duniani inategemea vijana katika kupata Maendeleo hivyo
serikali haitawaacha nyuma vijana katika sekta ya Kilimo na biashara.
Amewataka vijana
kuwa na mwamko wa elimu huku wengine wakiwa wataalam katika fani
mbalimbali jambo ambalo litawatafanya kuwa chachu ya Kilimo na
biashara na kufanya vijana waliokata tamaa kuingia katika sekta hiyo.
Amesema takwimu
zinaonyesha asilimia 53 ndio wanatumia jembe la mkono katika kilimo huku
asilimia 27 wakitumia wanyama katika kuendesha katika kuendesha kilimo
chao wakati takwimu zinaonyesha asilimia 20 wanatumia trekta .
Nae Mwenyekiti wa
Kongamano la Vijana Kimataifa Kuhusu Kilimo Biashara Majabi Emmanuel
amesema kuwa wanatarajia kuwa na washiriki 1000 kutoka sehemu mbambali
wa ndani na nje ya nchi.
Amesema kuwa
wameandaa Kongamano hilo kutokana na vijana kujitenga katika kilimo
wakati ndio chenye fursa ya kujiajiri moja kwa moja.
No comments:
Post a Comment