Bi Neema Kiure Mssusa kutoka
kampuni ya Ukaguzi wa mahesabu ya Ernst & Young na mwanachama wa
Taasisi ya TAWCA Tanzania Association Of Wome Cestfied Accountant
kushoto na Bi. Tumaini Lawrence Mkurugenzi Mtendaji wa (TAWCA) wa pili
kutoka kushoto na wenzao wakikabidhi vitabu mbalimbali vya mahesabu kwa
Angalo Izungo Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Triani wilayani Kinondoni
jijini Dar es salaam ikiwa ni msaada walioutoa kwa shule hiyo kwa ajili
ya watoto wanaosoma masomo ya hesabu.
Bi Neema Kiure Mssusa kutoka
kampuni ya Ukaguzi wa mahesabu ya Ernst & Young na mwanachama wa
Taasisi ya TAWCA Tanzania Association Of Wome Cestfied Accountant
kushoto na Bi. Tumaini Lawrence Mkurugenzi Mtendaji wa (TAWCA) wa pili
kutoka kushoto na wenzao wakikabidhi boksi la vitabu mbalimbali vya
mahesabu kwa Angalo Izungo Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Triani wilayani
Kinondoni jijini Dar es salaam na mmoja wa wanafunzi wanaosoma shuleni
hapo ikiwa ni msaada walioutoa kwa shule hiyo kwa ajili ya watoto
wanaosoma masomo ya hesabu.
Bi Neema Kiure Mssusa kutoka
kampuni ya Ukaguzi wa mahesabu ya Ernst & Young na mwanachama wa
Taasisi ya TAWCA Tanzania Association Of Wome Cestfied Accountant
akikabidhi vitabu vya hesabu kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya
Turiani Wilayani Kinondoni kushoto ni Bi. Tumaini Lawrence Mkurugenzi
Mtendaji wa (TAWCA) na wanachama wenzao wakishuhudia tukio hilo.
Wanachama wa Tanzania Association
Of Wome Cestfied Accountant (TAWCA)wakiwa katika picha na wanafunzi wa
shule hiyo mara baada ya kukabidhi msaada wa vitabu hivyo.
Wanachama wa Tanzania Association
Of Wome Cestfied Accountant (TAWCA) wakiwa katika picha ya pamoja mara
baada ya kukabidhi vitabu hivyo.
…………………………………………………………………………………………
TAASISI ya Wanawake Wahasibu
Tanzania(TAWCA)wametoa msaada wa vitabu mbalimbali vya hesabu na masomo
ya biashara vyenye thamani ya Sh.milioni 8.5 kwa Shule ya Sekondari
Turiani jijini Dar es Salaam.
Uamuzi wa TWCA kutoa msaada huo
kwenye shule hiyo ni kuwahamasisha wanafunzi hasa
wa kike kupenda masomo
ya hesabu nchini ili baadae waje kuongeza idadi ya watalaamu wahasibu
nchini.
Akizungumza leo shuleni hapo
wakati wa tukio la kukabidhi msaada huo, Mkurugenzi wa Taasisi ya
Wanawake Wahasibu Tanzania Tumaini Lawrence amesema wanawake wahasibu
nchini wameona haja ya kushiriki kwa vitendo kuhamasisha wanafunzi
kusoma masomo yanayohosu hesabu na ndio maana wameamua kutoa msaada huo
wenye lengo la kuwahamasisha wanafunzi wa kike nchini kupenda hesabu.
“Wanawake wahasibu nchini kwa
umoja wetu tumeamua kuchangishana fedha ili kufanikisha msaada huu kwa
ajili ya wanafunzi wa Sekondari ya Turiani.Tumekuja kuwahamasisha wasome
kwa bidi masomo ya hesabu na biashara ili tuongeze idadi ya wahasibu na
hawa wahasibu wa kike katika nchi yetu ambapo kwa sas idadi yao ni
chini ya asilimia 25 ya wahasibu wote.
“Kuna dhana ambayo inajengeka
kuwa masomo ya hesabu ni kwa ajili ya wanafunzi wa kiume tu lakini sisi
wahasibu wanawake ambao ndio mama zenu tunawaambia wanafunzi kuwa somo
la hesabu ni la wote.Hivyo wanafunzi wa kike jitahidi kusoma hesabu na
masomo ya biashara,”amesema Lawrence.
Kuhusu mikakati ya taasisi ya
wahasibu nchini, Lawrence amesema ni kuendelea kuhamasisha watoto wa
kike kupenda masomo ya hesabu na huku akitoa ushauari kwa wazazi na
walezi kuwajengea uwezo wa kujiamini watoto hao.
“Naomba nisieleweke vibaya ila
wahasibu wanawake wakiwa kwenye maeneo yao ya kazi wanakuwa waaminifu
sana.Kwa kutambua hilo ni jukumu letu kuwatia moyo wanafunzi wa kike
nchini kupenda hesabu,” Lawrence.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya taasisi hiyo Neema Msusa amesema ni faraja kwao kufika shuleni hapo kuzungumza na wanafunzi hao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya taasisi hiyo Neema Msusa amesema ni faraja kwao kufika shuleni hapo kuzungumza na wanafunzi hao.
“Tumefika shuleni hapa kwa lengo
la kumsha ari kwa wanafunzi wetu wa kike kusoma masomo ya
biashara.Tunawaambia hesabu haikimbiliki, hivyo wasome kwa bidi kwani
tunaona faida ya kusoma hesabu maana wanawake wahasibu kila mmoja yupo
kwenye taasisi anafanya kazi yake vizuri,”amesema
Ameongeza wao kuwa wahasibu
kumetokana na msingi mzuri ambao uliwekwa na walimu wao kuanzia ngazi ya
chini , hivyo wanaamini wanafunzi wa kike watasoma kwa bidi masomo ya
hesabu.
Wakati huo huo Mwalimu Mkuu wa
Shule ya Sekondari Turiani jijini Dar es Salaam Angalo Izungo amesema
anashukuru kupata msaada huo na kwamba wahasibu hao wanawake wameonesha
upendo wa dhati kwa shule yao.
Amefafanua changamoto kubwa iliyopo shuleni hapo ni vitabu vya masomo ya hesabu na biashara pamoja a uhaba wa walimu , hivyo baada ya kupata vitabu ombi lao ni Serikali kuwapatia walimu kwani waliopo ni wawili tu na wanafunzi walionao ni 506.
Amefafanua changamoto kubwa iliyopo shuleni hapo ni vitabu vya masomo ya hesabu na biashara pamoja a uhaba wa walimu , hivyo baada ya kupata vitabu ombi lao ni Serikali kuwapatia walimu kwani waliopo ni wawili tu na wanafunzi walionao ni 506.
“Tunao walimu wawili tu wa masomo
ya hesabu hapa shuleni kwetu, hivyo tunashukuru kwa msaada huu.Tunaomba
Serikali yetu ituongezee walimu wa masomo ya hesabu shuleni kwetu,
wanafunzi wetu wanapenda hesabu sana,”amesema Izungo.
No comments:
Post a Comment