Mkurugenzi wa ORCI, Mkurugenzi wa
Mipango hospitali ya Ocean Road Cancer Institute (ORCI), Dk.Daudi
Maneno akizungumza wakati akifungua semina ya waandishi wa habari kuhusu
magonjwa ya saratani iliyofanyika leo hospitalini hapo jijini Dar es
salaam kushoto ni Dk. Maguha Stephano.
Mkurugenzi wa Kinga na Daktari
Bingwa wa Magonjwa ya Saratani ORCI, Crispin Kahesa akitoa mada katika
semina hiyo iliyofanyika leo kwenye hospitali ya Ocean Road.
Daktari Bingwa wa magonjwa ya Saratani Dk. Sikudhani Muya akitoa mada kwa waandishi wa habari wakati wa semina hiyo.
……………………………………………………………………………….
Mkurugenzi wa Kinga na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani ORCI, Crispin Kahesa amesem taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Afya na
Sayansi Shirikishi cha Muhimbili
imefanikiwa kutoa mafunzo kwa wanafunzi 38 wa Shahada ya Kwanza ya Tiba
ya Mionzi (Bachelor of Science in Radiation Therapy Technology) huku
ikitoa mafunzo wanafunzi 26 wa Shahada ya Uzamili ya Onkolojia
(Masters of Medicine in Clinical Oncology). Mkurugenzi wa Kinga na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani ORCI, Crispin Kahesa amesem taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Afya na
Daktari Crispin Kahesa ameyasema
hayo leo Januari 31, wakati wa akiwasilisha mada kwenye semina ya siku
moja kwa waandishi wa habari kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Saratani
Duniani iliyofanyika hospitalini hapo.
Amesema mafunzo hayo yameongeza
uwepo wa wataalamu wa huduma za Saratani katika taasisi hapa nchini
ambapo kwa sasa Taasisi ina madaktari bingwa wa Onkolojia 25,
ikilinganishwa na madaktari bingwa 5 waliokuwepo mwaka 2010.
“Kuanzishwa kwa programu ya
Shahada ya Uzamili ya Onkolojia (Masters of Medicine in Clinical
Oncology) nchini kumeongeza ushirikiano na nchi za nje ambazo zimekuwa
zikileta wanafunzi kwa ajili ya mafunzo mbalimbali hapa nchini”
Ameongeza .
Amesema hadi kufikia Desemba
2018 programu hiyo ilikuwa imefundisha madaktari 17 ambapo kutoka
nchini Kenya walikuwa (8) kutoka Rwanda walikuwa (5), DRC alikuwa
mmoja (1), Nigeria alikuwa mmoja (1), Ethiopia mmoja (1), na Comoro
alikuwa mmoja (1) pia.
Taasisi ya Ocean Road pia
imetumia wigo huo wa ushirikiano kutangaza huduma mbalimbali
zinazotolewa hapa nchini hivyo kuvutia wagonjwa kutoka nchi hizo kuja
nchini kwa ajili ya kupata huduma za matibabu.
“Tunajukumu la kuhakikisha
tunatoa huduma za kinga na tiba na kutoa elimu kwa umma ya kujikinga na
magonjwa haya na kuendesha program za mafunzo kwa wataalamu na kufanya
tafiti mbalimbali,” amesema.
Amesema eneo jingine ambalo
serikali imewekeza ni upande wa tiba ambapo sasa wamepata mashine ya
LINAC zinazotibu kisasa zaidi magonjwa hayo katika mfumo wa 3D.
“Matokeo ya tiba kwa mashine hizi
ni bora zaidi kuliko mashine ambazo tulikuwa tunazitumia hapo awali,
tumeweza kupunguza muda wa magonjwa kisubiri matibabu kutoka wiki sita
hadi chini ya wiki nne,” amebainisha.
Ameongeza “Haya ni mafanikio makubwa kwetu, kuweza kuendelea kupunguza muda wa wagonjwa kusubiri huduma.
Daktari Crispin Kahesa ameongeza
kuwa wanaishukuru Serikali kwa jinsi ambavyo imekuwa ikifanya jitihada
mbalimbali na kutoa fedha ili kuwezesha taasisi ya (Ocean Road Cancer
Intitute) kuendelea kutoa huduma kwa ufanisi jambo ambalo linawajenga
kiutendaji na kuwapa hamasa ya kuchapa kazi.
Naye daktari Bingwa wa Magonjwa
ya Saratani ORCI, Maguha Stephano amesema maadhinisho ya Siku ya
saratani hufanyika Februari 4, kila mwaka.
“Hupewa kauli mbiu kwa kipindi
cha miaka mitatu mitatu, kwa mwaka 2019 hadi 2021 inasema ‘Mimi
Ninaweza, Nitapiga Vita Saratani’, katika kuiadhimisha tunafanya
uchunguzi wa awali bila malipo, tunawasihi wananchi wajitokeze kwa wingi
ili kuja kujua afya zao,” amesema.
No comments:
Post a Comment