Na Saidina Msangi, WFM, Dodoma
Serikali iliwalipa stahili
zote Watumishi wa Kiwanda cha nguo cha KILITEX kilichopo mkoani Arusha
baada ya kufungwa kutokana na tatizo la ukosefu wa mtaji na malimbikizo
ya madeni.
Hayo yamebainishwa Bungeni
Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji,
alipokua akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalaum Mhe.
Catherine Magige, aliyeuliza ni lini Serikali itawalipa wafanyakazi 545
wa KILITEX ambao bado wanadai pensheni baada ya kiwanda hicho kufungwa
ilihali mwajiri wao hakuwasilisha michango yao kwenye Mfuko wa Kijamii
wa PPF.
Dkt. Kijaji alisema kuwa,
kwa mujibu wa kumbukumbu na nyaraka za ufilisi, taratibu za ufilisi
zilikamilika na wafanyakazi hao walilipwa stahiki zao kwa mujibu wa
Sheria ya Makampuni namba 46 ya mwaka 1931.
“Baadhi ya wafanyakazi
walilipwa mafao ya kiinua mgongo kwa mkupuo na wengine walirejeshewa
michango yao kwa kadiri walivyochangia baada ya Mfilisi kushindwa kulipa
riba, adhabu na malimbikizo ya michango kwenye mfuko wa Pensheni wa
PPF”, alisema Dkt. Kijaji.
Alisema Kiwanda hicho kilisimamisha shughuli za uzalishaji mwaka 1994 na kuwekwa chini ya ufilisi na PSRC mwaka 1995.
Aidha akijibu swali la
nyongeza la Mbunge wa Mlimba, Mhe. Suzan Kiwanga, alietaka kufahamu ni
lini wafanyakazi 11075 wa Shirila la Reli la Tanzania na Zambia- TAZARA
waliostaafishwa kwa lazima miaka 55 mwaka 2005, watalipwa mafao yao.
No comments:
Post a Comment