Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza katika mazishi ya Hidaya Omar, mke wa Mufti wa Tanzania,
Abubakary Zubier yaliyofanyika katika kijiji cha Kwamdolwa wilayani
Korogwe, Januari 31, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa akishiriki katika sala ya jeneza wakati wa mazishi ya Hidaya
Omar, Mke wa Mufti wa Tanzania, Abubakary Zubeir (kushoto kwa Waziri
Mkuu) yaliyofanyika katika kijiji cha Kwamdolwa wilayani Korogwe,
Januari 31, 2019. Kulia kwa Waziri Mkuu ni Sheikh Mohammed Kigoda
aliyeongoza sala hiyo na kushoto ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es
salaam, Alhad Mussa Salum.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiagana na Mufti wa Tanzania, Abubakary Zubeir baada ya kushiriki
katika mazishi ya Hidaya Omar, mke wa Mufti ,yaliyofanyika katika
kijiji cha Kwamdolwa wilayani Korogwe, Januari 31, 2019. Katikati ni
Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhad Mussa Salum. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
………………..
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa
amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika mazishi ya mke wa Mufti na
Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Aboubakary Bin Zubeir yaliyofanyika
Kwamndolwa, Korogwe mkoani Tanga.
Akitoa salam kwa niaba yake
amesema “Rais Dkt. Magufuli aliweka nia ya dhati kushiriki mazishi haya
ila kwa bahati mbaya leo ana mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya
Afrika Mashariki unaofanyika jijini Arusha ambapo yeye ni Mwenyekiti.”
“Mheshimiwa Rais amenituma nije
nikupe pole wewe, watoto, familia na wote walioguswa na msiba huu.
Mheshimiwa Rais anawaombea kwa Mungu ili mpate utulivu katika kipindi
hiki kigumu cha kuondokewa na nguzo katika familia. Haya yote ni mapenzi
ya Mwenyezi Mungu.”
Waziri Mkuu ameshiriki mazishi hayo ya mke wa Mufti, Bibi Hidaya Omar leo (Alhamisi, Januari 31, 2019).
Kadhalika, Waziri Mkuu amewasihi
wafiwa na waombolezaji wote waendelee kuwa watulivu na kumuombea
marehemu kila mmoja kwa imani yake ili Mwenyezi Mungu ailaze roho ya
marehemu mahala pema.
Kwa upande wake, Sheikh wa Mkoa wa
Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum akizungumza kwa niaba ya
familia amemshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kumtuma Waziri Mkuu
amuwakilishe katika mazishi hayo. Pia amewashukuru watu wote
waliojitokeza kwa ajili ya kuifariji familia kutokana na msiba
walioupata.
Viongozi wengine waliohudhuria
mazishi hayo niWaziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto,Mhe. Ummy Mwalimu, Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo,
Mhe. Salma Kikwete, Mhe. Hawa Ghasia, Mhe. Mary Chatanda ,Mhe. Mkuu wa
Mkoa wa TangaMartine Shigelana Masheikh wa Mikoa.
No comments:
Post a Comment