Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Hussein
Laay wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari ya
Kassim Majaliwa iliyopo Kata ya Nachingwea katika Halmashauri ya wilaya
ya Ruangwa kuzindua madarasa mawili yaliyojengwa na Benki hiyo kwa
gharama ya shilingi milioni 80, Desemba 31, 2018. Kushoto ni Mkurugenzi
Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
kisalimiana na baadhi ya viongozi na watendaji wa Benki ya CRDB wakati
alipowasili kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kassim
Majaliwa kuzindua madarasa mawili yaliyojengwa na benki hiyo kwenye
Kata ya Nachingwea katika Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa kwa gharama
ya Shilingi milioni 80, Desemba 31, 2018. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi
ya Benki ya CRDB, Ally Hussein Laay na watatu kulia ni Mkurugenzi
Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizindua madarasa mawili yaliyojengwa na Benki ya CRDB kwa gaharama ya
shilingi milioni 80 katika Shule ya Sekondari ya Kassim Majaliwa kwenye
Kata ya Nachingwea iliyopo katika Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa,
Desemba 31, 2018. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu,
Mary Majaliwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Hussein Laay,
Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela na kulia ni Mkuu wa
wilaya ya Ruangwa, Hashim Ngandirwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizindua madarasa mawili yaliyojengwa na Benki ya CRDB kwa gaharama ya
shilingi milioni 80 katika Shule ya Sekondari ya Kassim Majaliwa iliyopo
Kata ya Nachingwea katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Desemba 31,
2018. Kulia ni Mkewe Mary, wapili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya CRDB,
Ally Hussein Laay na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid
Nsekela. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na
Mkewe Mary (watatu kushoto) wakiwa katika moja ya madarasa mawili
yaliyojengwa na Benki ya CRDB kwa gaharama ya shilingi milioni 80 katika
Shule ya Sekondari ya Kassim Majaliwa iliyopo Kata ya Nachingwea katika
Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa na kuzinduliwa na Waziri Mkuu, Desemba
31, 2018. Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa
CRDB, Abdulmajid Nsekela, Mwanfunzi wa Kidato cha Pili katika Shule
hiyo, Mwanahawa Choni, Khadija Abdallah wa Kidato cha Pili katika Shule
hiyo na Mwenyekiti wa Bodi ya CRDB, Ally Hussein Laay. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Hussein Laay
(kushoto kwake) kukagua madarasa mawili aliyoyazindua katika Shule ya
Sekondari ya Kassim Majaliwa iliyopo kwenye Kata ya Nachingwea katika
Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Desemba 31, 2018. Madarasa hayo
yamejengwa na CRDB kwa gharama ya shilingi milioni 80. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Waalikwa wakimsikiliza Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kuzindua madarasa
mawili yaliyojengwa na Benki ya CRDB kwa gharama ya shilingi milioni 80
katika Shule ya Sekondari ya Kassim Majaliwa kwenye Kata ya Nachingwea
katika Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Desemba 31, 2018. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza baada ya kuzindua madarasa mawili yaliyojengwa na Benki ya
CRDB kwa gaharama ya shilingi milioni 80 katika Shule ya Sekondari ya
Kassim Majaliwa katika Kata ya Nachingwea kwenye Halmashauri ya Wilaya
ya Ruangwa, Desemba 31, 2018. Kushoto ni Mkewe Mary, Wapili kulia ni
Mwenyekiti wa Bodi ya CRDB, Ally Hussein Laay na kulia ni Mkurugenzi
Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza baada ya kuzindua madarasa mawili yaliyojengwa na Benki ya
CRDB kwa gaharama ya shilingi milioni 80 katika Shule ya Sekondari ya
Kassim Majaliwa katika Kata ya Nachingwea kwenye Halmashauri ya Wilaya
ya Ruangwa, Desemba 31, 2018. Kushoto ni Mkewe Mary, Wapili kulia ni
Mwenyekiti wa Bodi ya CRDB, Ally Hussein Laay na kulia ni Mkurugenzi
Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
………………………………………………………………………
WAZIRI MKUU, Kassim
Majaliwa amepokea msaada wa vyumba viwili vya madarasa vikiwa
na
madawati vyenye thamani ya sh. milioni 80 kutoka kwa bank ya CRDB.
Alipokea madarasa hayo jana
(Jumatatu, Desemba 31, 2018) katika shule ya Sekondari Kassim Majaliwa
iliyopo Kata ya Nachingwea katika wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi
Waziri Mkuu aliushukuru uongozi
wa benki ya CRDB kwa msaada hu ambao umesaidia kupunguza changamoto ya
upungufu wa madarasa unaoikabili wilaya hiyo.
Kadhalika, Waziri Mkuu alizitaka
taasisi nyingine ziige mfano wa bank ya CRDB kwani imekuwa bega kwa bega
na Serikali katika kuchangia shughuli za kimaendeleo nchini.
Hata hivyo, Waziri Mkuu alitoa
wito kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Kassim Majaliwa kutumia vizuri
madarasa hayo na kutunza mali zilizopo shuleni hapo.
Alisema ujenzi wa shule hiyo ni
mradi uliobuniwa na wakazi wa kata ya Nachingwea ili kuwawezesha watoto
wao kupata elimu katika eneo lililo karibu na makazi yao.
Waziri Mkuu alisema awali
wanafunzi wa kata hiyo walikuwa wanatembea umbali mrefu hadi shule ya
sekondari ya Ruangwa jambo ambalo lilikuwa ni changamoto kwao.
“Nawaomba wananchi wenzangu
tuendelee kushirikiana katika kuibua na kubuni miradi mbalimbali kwa
ajili ya kuboresha maendeleo kwenye kata yetu ya Nachingwea.”
Pia Waziri Mkuu alikabidhi
kompyuta 20 kwa shule za sekondari tano ambazo ni Kassim Majaliwa,
Likunja, Mnacho, Hawa Mchopa na Ruangwa.
Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema benki yao inathamini elimu na
imekuwa ikirudisha kwa jamii faida wanayoipata kwa kuchangia shughuli za
maendeleo.
Alisema mbali na msaada huo wa
vyumba viwili vya madarasa pamoja na madawati yake, pia aliahidi kutoa
sh. milioni 20 ili zitumike kununulia madawati yatakayosaidia kupunguza
changamoto ya madawati wilayani Ruangwa.
Kwa upande wao, wakazi wa kata ya
Nachingwea wilayani Ruangwa waliishukuru Serikali kwa kuwaunga mkono
katika mradi wa ujenzi wa shule hiyo ya sekondari ambayo imewawezesha
watoto wao kusoma karibu na maeneo yao ya makazi yao.
Mmoja wa wakazi hao Omari Losi
alisema ujenzi wa shule hiyo utawarahisishia wanafunzi kwenda shule na
kuwaondolea shida ya kutembea umbali mrefu kwenda shule ya sekondari ya
Ruangwa walikokuwa wakisoma awali.
Naye, mkazi mwingine wa kata hiyo
ya Nachingwea, Mariam Kingamkono alisema uwepo wa shule ya sekondari
katika kata yao kumeongeza hamasa ya wanafunzi kupenda kusoma kwa sababu
wameondolea shida ya kutembea umbali mrefu.
Alisema shule hiyo inawalimu
wazuri na wa kutosha na ina mazingira mazuri ya kujifunzia, hivyo
aliwaomba wazazi wenzake waendelee kushirikiana na Serikali katika
kuboresha maendeleo kwenye kata yao hususan ujenzi wa shule.
No comments:
Post a Comment