RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Afisa
Masoko wa Shirika la Biashara la Taifa (ZSTC) Nassor Salum Nassor,
wakati akitembelea maonesho ya Bidhaa za ZSTC wakati wa maadhimisho ya
50 zilizofanyika katika viwanja vya Hotel Verde Mtoni Zanzibar,kushoto
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,Mke waMakamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman, Makamu Pili wa Rais wa Zanzibar
Mhe. Balozi Seif na Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mhe. Balozi
Amina Salumu Ali, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya hotel Verde
jana usiku.
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama
Mwanamwema Shein, akisalimiana na Mama Fatma Karume, wakati akiwasili
katika ukumbi wa hafla ya sherehe za kuadhimisha Miaka 50 ya ZSTC
zilizofanyika katika viwanja vya Hoteli Verde Mtoni Zanzibar, jana
usiku.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Iddi na Mama Mwanamwema Shein, na
Viongozi wengi wakiwa wamesimama wakati ukiimbwa wimbo wa Taifa na
Kikundi cha Taifa cha Taraab Zanzibar, jana usiku katika hoteli ya Verde
Mtoni
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, kushoto Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, Mkuu wa Mkoa wa Mjini
Magharibi Unguji Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud na kulia Waziri wa BiashaRA
NA Viwanda Zanzibar,Mhe Balozi Amina Salum Ali na Mke wa Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman, wakifuatilia onesho la “
Documentary “ ya Miaka 50 ya ZSTC,hafla hiyo imefanyika katika viwanja
vya hotel Verde Mtoni Zanzibar, jana usiku.
WADAU wa ZSTC wakifuatilia hafla
hiyo ya Maadhimisho ya sherehe za Miaka 50 ya Shirika hilo tangu
kuazishwa kwake Zanzibar 1968, zilizoadhimishwa katika viwanja vya
Hoteli Verde Mtoni Zanzibar, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar Mhe. Dk.
Shein, akihutubia hafla hiyo, jana usiku.
WASANII wa Kikundi wa Kikundi cha
Kachara kutoka kisiwani Pemba wakitowa burudani wakati wa sherehe za
kuadhimisha Miaka 50 ya ZSTC zilizofanyika jana usiku katika viwanja vya
Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.2-12-2018
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akikata Keki Maalum ya
miaka 50 ya Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) kulia Waziri wa
Biashara na Viwanda Zanzibar Mhe. Balozi Amina Salum Ali na Mwenyekiti
wa Bodi ya ZSTC Ndg.Kassim Ali na kushoto Mkurugenzi Muendeshaji wa
(ZSTC)Dkt. Said Seif Mzee, Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda Mhe.
Hassan Hafidh na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Viwanda Ndg. Ali
Juma, wakisherehekea wakati wa hafla hiyo ya ukataji wa Keki Maalum ya
Miaka 50 ya ZSTC, katika viwanja vya hoteli Verde Mtoni Zanzibar, hafla
hiyo imefanyika jana usiku.2-12-2018.
MWENYEKITI wa Bodi ya Shirika la
Bishata la Taifa Zanzibar (ZSTC) Ndg. Kassim Ali, akisoma taarifa ya
mafanikio ya Shirika hilo wakati wa hafla ya kuadhimisha Miaka 50 ya
ZSTC zilizofanyika jana usiku katika viwanja vya hoteli ya Verde Mtoni
Zanzibar.
WAZIRI wa Biashara na Viwanda
Zanzibar Mhe. Balozi Amina Salum Ali, akimkabidhi zawadi Maalum Mdau wa
Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar, (ZSTC) Ndg.Tarun. Pandey, kutoka
Kampuni ya Afcom Trading dmcc, kutoka Nchini Dubai.wakati wahafla hiyo
ya kuadhimisha Miaka 50 ya ZSTC zilizofanyika jana usiku katika viwanja
vya Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia na kutowa
nasaha zake kwa Uongozi wa ZSTC na wananchi waliohudhuria hafla ya
kuadhimisha Miaka 50 ya Shirika hilo zilizofanyika jana usiku katika
viwanja vya hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.2-12-2018.(Picha na Ikulu)
No comments:
Post a Comment