Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akihutubia wanachi wa Kenya na Tanzania katika eneo la
Mpakani Namanga mara baada ya hafla ya ufunguzi wa Kituo cha Kutoa huduma kwa
pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Tanzania na Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati wa
kupiga picha za pamoja mara baada ufunguzi wa Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja
mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Tanzania na Kenya.
Rais wa Kenya
Uhuru Kenyatta akihutubia wanachi wa Kenya na Tanzania katika eneo la
Mpakani Namanga mara baada ya hafla ya
ufunguzi wa Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post
(OSBP) upande wa Tanzania na Kenya.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa
Oldonyo Sambu Wilayani Arumeru wakati akitokea Namanga mpakani mwa Tanzania na
Kenya. PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakipungia
wananchi mara baada ya kuwasili katika eneo la mkutano pembezoni mwa Kituo cha
Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa
Tanzania.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi funguo Rais wa
Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kufungua Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja
mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Tanzania
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea funguo kutoka kwa
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kufungua Kituo cha Kutoa huduma kwa
pamoja mpakani Namanga One Stop Border Post (OSBP) upande wa Kenya.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakikata utepe
kuashiria ufunguzi wa Kituo cha Kutoa huduma kwa pamoja mpakani Namanga One
Stop Border Post (OSBP) upande wa Kenya.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na watoto
wawili kutoka Kenya waliofika kumpokea katika kituo cha kutoa huduma kwa pamoja
kwa upande wa Kenya.
Baadhi ya Wananchi wa Kenya na Tanzania
waliohudhuria katika hafla ya ufunguzi wa vituo hivyo Mpakani Namanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakielekea
upande wa mpaka wa Tanzania mara baada ya ufunguzi wa kituo cha kutoa huduma
kwa pamoja kwa upande wa Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakielekea
kupanda gari moja kutoka Arusha mjini kuelekea Namanga mpakani mwa Tanzania na
Kenya. (PICHA NA IKULU)
Na
Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.
Mhe. Rais Dkt. John
Pombe Magufuli amesema kituo kipya cha ukaguzi Namanga kinatarajia kuingizia
Tanzania Shilingi Bil. 58 mwaka huu wa fedha, 2018/2019.
Rais Magufuli
ameyasema hayo leo Namanga, Jijini Arusha wakati wa ufunguzi wa kituo
hicho uliofanyika mpakani mwa Tanzania na Kenya.
Rais Magufuli
amesema, kukamilika kwa kituo hicho kumeongeza mapato kutoka wastani wa
shilingi Bil. 3 kwa mwezi hadi shilingi Bil. 4.5 kwa mwezi ambapo kwa mwaka huu
wa fedha Serikali ya Tanzania inatarajia kukusanya jumla ya shilingi Bil. 58
kutoka katika kituo hicho.
"Ujenzi wa
vituo vya huduma za pamoja mipakani vimerahisha huduma za usafiri na kupunguza
gharama za muda.Zamani watu walikuwa wakitumia siku nzima kuvuka mpaka, lakini
sasa hivi mtu anatumia dakika 15 tu kuvuka mpaka huo," amesema Rais
Magufuli.
Amesema, kituo
hicho kitawawezesha wafanyabiashara kuvusha bidhaa zao zaidi ya mara Kumi
kwa mwezi tofauti na ilivyokuwa mwanzo ambapo ilikuwa nadra kwa mfanyabiashara
kuvuka mpaka huo hata mara Nne kwa mwezi.
Aidha amesema,
kituo hicho kitaimarisha shughuli za biashara na utalii kwa nchi zote mbili
kutokana na kurahisishwa kwa huduma ya usafiri pamoja na miundombinu mingine
katika kituo hicho.
Kwa upande wake,
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta amesema ni jukumu lao viongozi
kuhakikisha wananchi wanafanyabiashara bila kupingwa na waweze kuimarisha
biashara kati ya nchi hizo mbili.
Amesema dhumuni la
ujenzi wa kituo hicho ni kuwarahisishia wafanyabiashara wadogo na wakubwa
kufanya biashara zao kwa urahisi, ili kila mwana jumuiya wa Afrika Mashariki
aweze kunufaika na umoja huo.
Aidha amewataka
wale wote waliopewa jukumu la kusimamia kituo hicho basi wajue kazi yao sio
kumnyanyasa mwananchi bali kumsaidia mwananchi afanye biashara yake. Pia
wananchi wajue kuwa wakisaidiwa kufanya biashara hawajaambiwa kufanya biashara
ya madawa ya kulevya, kuua wanyama au biashara ya magendo bali wanatakiwa
kufanya biashara ya haki ili mtu apate fedha yake ya haki.
Nae, Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe Balozi Dkt. Augustine
Mahige amesema, kuwa na kituo kimoja cha forodha na uhamiaji kinaboresha soko
la pamoja la Afrika Mashariki.
Vile vile amesema,
baada ya soko la pamoja, Jumuiya ya Afrika Mashariki inajiandaa kuwa na sarafu
moja ifikapo 2020.
Kituo cha pamoja
Namanga kimejengwa kwa ufadhili wa nchi ya Japani kupitia Shirika la Maendeleo
la JICA ambapo kwa upande wa Tazania jumla ya shilingi Bil. 18.6 zimegharamiwa
. Aidha Benki ya Maendeleo ya Afrika imefadhili kiasi cha Dola za Marekani
117,000 kwa ajili ya kuweka vifaa vya ofisi kwa upande wa Tanzania na Kenya.
No comments:
Post a Comment