Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu
Kazungu (kulia) akisikiliza maelezo ya namna Chuo cha Mipango ya
Maendeleo Vijijini inavyotekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo vijijini yenye
lengo la kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii ikiwemo mazingira,
wakati wa Mahafali ya 32 yaliyofanyika katika Kampasi ya Dodoma.
Mlau wa Mahafali ya 32 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini
Dkt. Christina Mandala, akiongoza maandamano wakati wa mahafali ya 32 ya Chuo
hicho yaliyofanyika katika Kampasi ya Dodoma, ambapo wahitimu 2596 wametunukiwa
vyeti na shahada mbalimbali. Kulia ni Kaimu Mkuu wa chuo hicho Prof. Hozen
Mayaya na kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi chuoni hapo Bi.
Mugabe Mtani.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatib Kazungu
akihutubia wahitimu na wageni mbalimbali waliohudhuria katika mahafali ya 32 ya
Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini yaliyofanyika katika Kampasi
ya Chuo hicho, Dodoma.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Prof.
Hozen Mayaya, akitoa taarifa ya maendeleo ya Chuo kwa wahitimu na wageni
mbalimbali waliohudhuria katika mahafali ya 32 ya Chuo
hicho yaliyofanyika katika Kampasi ya Chuo, Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu
akimtunuku Shahada ya Uzamili, mmoja wa wahitimu katika mahafali ya 32 ya chuo
cha Mipango ya Maendeleo Vijijini yaliyofanyika katika Kampasi ya chuo hicho,
Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu
Kazungu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya 32 ya Chuo cha Mipango ya
Maendeleo Vijijini akitunuku wahitimu wa kada mbalimbali
katika mahafali hayo kampasi ya Dodoma.
Wahadhili wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Prof. Youze
Mnguu (kushoto) na Prof. Zacharia Masanyiwa, wakifuatilia kwa makini matukio
wakati wa Mahafali ya 32 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo
Vijijini akitunuku wahitimu wa kada mbalimbali katika
mahafali hayo Kampasi ya Dodoma
Baadhi ya wahitimu wa kada mbalimbali katika chuo cha Mipango ya
Maendeleo Vijijini wakiwa katika sherehe za mahafali ya 32 ya chuo
hicho yaliyofanyika chuoni hapo Jijini Dodoma.
Baadhi ya wahitimu wa kada mbalimbali katika Chuo cha Mipango ya
Maendeleo Vijijini wakipunga kofia zao kwa furaha wakati wa Mahafali ya 32
yaliyofanyika chuoni hapo, Jijini Dodoma.
Baadhi ya wahitimu wa Shahada ya Uzamili katika Chuo cha
Maendeleo Vijijini wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya
Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu, wakati wa Mahafali ya
32 yaliyofanyika chuoni hapo Jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment