Msanii wa Filamu, Wema Sepetu,
leo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es
Salaam akisubiri kusomewa mashtaka ya kusambaa mitandaoni kwa video zake
za faragha.
Wema amefikishwa mahakamani
hapo leo Alhamisi, Novemba 1, 2018,majira ya saa 4 asubuhi akiwa amevaa
miwani na kujitanda ushungi huku akisindikizwa na askari wawili ambapo
alipelekwa kwenye chumba cha mahabusu cha mahakama hiyo.
Jana taarifa zilisambaa mitandaoni
kuwa msanii huyo ambaye ni mshindi wa Taji la Miss Tanzania Mwaka 2006,
alikuwa amekamatwa na polisi lakini taarifa hizo hazikuthibitishwa.
Hivi karibuni msanii huyo
alisambaza mitandaoni video zake za faragha akiwa na mpenzi wake,
anayejulikana kama PCK. Licha ya kuomba radhi siku chache baadaye, Bodi
ya Filamu nchini ilimfungia msanii huyo kujihusisha na masuala ya sanaa
kwa muda usiojulikana huku ikisema adhabu yake halisi inakuja.
No comments:
Post a Comment