Pages

Thursday, November 1, 2018

WEMA SEPETU AFIKISHWA MAHAKAMANI KISUTU




Msanii wa Filamu, Wema Sepetu,  leo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam akisubiri kusomewa mashtaka ya kusambaa mitandaoni kwa video zake za faragha.
Wema amefikishwa mahakamani hapo leo Alhamisi, Novemba 1, 2018,majira ya saa 4 asubuhi akiwa amevaa miwani na kujitanda ushungi huku akisindikizwa na askari wawili ambapo alipelekwa kwenye chumba cha mahabusu cha mahakama hiyo.
Jana taarifa zilisambaa mitandaoni kuwa msanii huyo ambaye ni mshindi wa Taji la Miss Tanzania Mwaka 2006, alikuwa amekamatwa na polisi lakini taarifa hizo hazikuthibitishwa.
Hivi karibuni msanii huyo alisambaza mitandaoni video zake za faragha akiwa na mpenzi wake, anayejulikana kama PCK. Licha ya kuomba radhi siku chache baadaye, Bodi ya Filamu nchini ilimfungia msanii huyo kujihusisha na masuala ya sanaa kwa muda usiojulikana huku ikisema adhabu yake halisi inakuja.

No comments:

Post a Comment