Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe.
Gelasius Byakanwa (mwenye shati Jeupe) akikagua ujenzi wa mfereji wa
maji kutoka Skoya, Nabwaba, Shakuru hadi Mtepwezi.
Mfereji wa kuondoa maji kutoka Skoya, Nabwada Shakuru hadi Mtepwezi
Ujenzi wa soko la Chuno
Na Evaristy Masuha – Mtwara
Serikali
kupitia mradi wa uendelezaji miji Mkakati (Tanzania Strategic Cities
Project) imetoa bilioni 21.7 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu
mbalimblai ya maendeleo katika Manispaa ya Mtwara mikindani. Miradi hiyo
ni pamoja na ujenzi wa barabara 4 za mitaa kwa kiwango cha lami, Ujenzi
wa maeneo matatu ya kupumzikia (Recreation Center), mfereji mkubwa wa
kuondoa maji ya mvua, ujenzi wa soko la kisasa pamoja na kituo cha
daladala eneo la Mikindani.
Akizungumza
leo wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi hiyo iliyofanywa na Mkuu wa
Mkoa wa Mtwara, Mkuu wa wilaya ya Mtwara Mhe. Evod Mmanda amesema fedha
hizo zimetolewa kwa mkopo na Benki ya dunia na kwamba ujenzi wa miradi
hiyo yote inatarajiwa kukamilika ifikapo Oktoba 2019.
Kwa upande
wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Byakanwa amesema
kukamilika kwa miradi hiyo kutaufanya mji wa mtwara kuwa na muonekano
mzuri na kwamba hiyo ndiyo hatua nzuri kuifanya Manispaa kuwa na sifa ya
kuwa Jiji.
“Naamini baada ya kukamilika miradi hii Mtwara itakuwa sehemu nyingine na pengine inaweza kupata sifa ya kuelekea kuwa jiji”.
Amewataka vijana waliopata nafasi ya kuajiliwa katika ujenzi wa miundombinu hiyo kuwa waamifu ili kujijengea imani kwa waajiri.
No comments:
Post a Comment