Mmoja
wa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam akipima tezi dume katika Hospitali
ya Taifa Muhimbili tawi la Mloganzila iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya
Ubungo. Kulia ni mtaalam wa radiolojia, Burhani Abdul akimpima tezi
dume kwa kutumia Utrasound.
Hospitali ya Taifa Muhimbili tawi la Mloganzila iliyopo Halmashauri ya Manispaa
Rais
wa Chama cha Wataalam wa Matumizi ya Mionzi katika uchunguzi na Tiba
Tanzania (TARA), Stephen Mkoloma akitoa elimu kwa wanaume kuhusu tezi
dume ikiwamo sababu, dalili na jinsi ya kujikinga.
Baadhi
ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wakisubiri kupima tezi dume katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili tawi la Mloganzila iliyopo Halmashauri ya
Manispaa ya Ubungo.
NA
JOHN STEPHENE, MNH
MAMIA ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam
leo wamejitokeza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tawi la Mloganzila
iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa ajili ya zoezi la kupima bure
tezi dume (prostate) na mfumo wa njia ya mkojo kwa kutumia ultrasound.
Zoezi hilo limeandaliwa na Hospitali ya
Muhimbili tawi la Mloganzila kwa kushirikiana na Chama cha Wataalam wa Matumizi
ya Mionzi katika uchunguzi na Tiba Tanzania (TARA) ikiwa ni maadhimisho ya wiki
ya wataalam wa mionzi tiba duniani.
Akizungumzia zoezi hilo mtaalam wa Radiolojia,
Dkt. Lulu Sakafu amesema umri unavyozidi kwenda juu, wanaume wanakuwa katika
hatari ya kupata matatizo ya tezi dume, hivyo wameshauriwa kujenga utamaduni
kwa kupima afya zao mara kwa mara.
Amesema watu wasiofanya mazoezi wako katika
hatari ya kupata matatizo ya tezi dume, wanaume wanaopenda kula chakula chenye
kiasi kikubwa cha mafuta na wengine wanaweza pata ugonjwa huo kutokana na
historia ya familia zao.“Katika maadhimisho ya mwaka huu tumeamua
kupima tezi dume kwa wanaume wenye umri kuanzia miaka 45 ili kuangalia dalili
na viashiria vya ugonjwa huu kwa sababu kansa ya tezi dume duniani inashika
nafasi ya tatu kwa kusababisha vifo kwa wanaume kutokana na saratani ya tezi
dume,” amesema Dkt. Sakafu.Akizungumzia dalili za tezi dume, Dkt. Sakafu
amesema kuwa kupata shida wakati wa haja ndogo, kutiririka kwa mkojo baada ya
kumaliza haja ndogo, kujisaidia mkojo wenye mtiririko dhaifu, kukojoa mara kwa
mara nyakati za usiku na kujikamua wakati wa kujisaidia na kushindwa kumali mkojo
wote.Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Tiba
Shirikishi Muhimbili, Dkt. Praxeda Ogweyo amesema wanaume wasiogope kujitokeza
kupima tezi dume kwa kuwa hivi sasa inatumika njia nyingine ya ultrasound
badala ya ile ya zamani ya vidole.Naye Rais wa TARA, Stephen Mkoloma ambaye ni
mtaalam wa radiolojia amesema wamechangua kupima tezi dume kwa kuwa takwimu za
wagonjwa wanaoripotiwa hospitali kutokana na matatizo ya tezi dume imeongezeka.“Nawashauri watu kupima afya zao mara kwa mara
ili kujua afya zao mapema kwani ukigundua ugonjwa mapema gharama za matibabu
zinakuwa chini kuliko kusubiri ugonjwa unapokuwa mkubwa au sugu,” amesema
Mkoloma.


No comments:
Post a Comment