Mkurugenzi
wa Uendeshaji, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Anselim Peter,
(kushoto), akimpongeza mgeni rasmi, Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na
Tathmini, Mamlaka ya
Usimamizi na
Udhibiti Sekta ya Hifadhi ya Jamii Nchini (SSRA), Bw. Joseph
Mutashubilwa, baada ya kufungua magfunzo ya Sheria ya Fidia kwa
Wafanyakazi yaliyowaleta pamoja viongozi na watendaji wa Chama cha
Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) na kufanyika mjini Morogoro
Oktoba 1, 2018.
Meza kuu katika picha ya pamoja na viongozi.
Bw.Mutashubilwa, (aliyesimama) akitoa hotuba hiyo. Kushoto ni Bw. Anselim Peter na kulia ni Katibu Mkuu wa TUGHE taifa, Bw.Henry Mkunda
NA
K-VIS BLOG, MOROGORO
Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Anselim Peter, akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu, akizunguzma kwenye ufunguzi huo.
Katibu Mkuu wa TUGHE taifa, Hery Mkunda, akizungumza mwanzoni mwa mafunzo hayo. |
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mafunzo hayo.
Bw. Peter (kulia) akijadiliana jambo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano WCF, Bi. Laura Kunenge
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada.
Mshiriki kutoka TUGHE Kilimanjaro, Simon E Msuya, akizungumza
Mshiriki kutoka mkoa wa Morogoro, …..akizungumza
Katibu Mkuu wa TUGHE, Bw. Hery akiuliza
swali kuhusu utaratibu wa kutoa mafao kwa mtu aliyepata ajali wakati
akitekeleza majukumu ya kazi ya mwajiri
Naibu Katibu Mkuu wa TUGHE taifa (Afya) Mhandisi Amani Msuya akizunhgumza
Mwakilishi toka Mkoa wa Tanga, Bi. Flora C Urassa akiuliza swali.
Mwakilishi toka Mkoa wa Mbeya, Bi.Janeth Masawe, akiulzia swali.
Bw. Rugemalira M. Rutatina, akiuuliza swali.
Mwakilishi toka Mkoa wa Pwani, Bw. Shadrack C. Mkodo akiuliza swali.
Mwakilishi wa TUGHE Mkoa wa Ruvuma Bw. Athanas B. Tarimo akiuliza swali.
Bw. Steven R. Wadi akiuliza swali, (kulia) ni Msimamizi na mjuongozaji wa semina Bi. Laura Kunenge.
Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Anselim Peter, (kushoto), akibadilishana mawazo na Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dodoma, Bw. Mchenya M. John
Meneja wa huduma za Sheria Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bw. Kitandu Ugula (kushoto), akibadilishana mawazo na Afisa Uhusiano na Uhamasishaji Mamlaka hiyo, Bi. Zawadi Msalla

Meza kuu katika picha ya pamoja kundi la kwanza
Meza kuu katika picha ya pamoja kundi la pili.
Meza kuu katika picha ya pamoja na viongozi.
Bw.Mutashubilwa, (aliyesimama) akitoa hotuba hiyo. Kushoto ni Bw. Anselim Peter na kulia ni Katibu Mkuu wa TUGHE taifa, Bw.Henry Mkunda
NA
K-VIS BLOG, MOROGORO
MKURUGENZI
Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti Sekta ya Hifadhi ya Jamii Nchini
(SSRA) Dkt. Irene Isaka, amewataka viongozi na watendaji wa Chama cha
Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) kuhakikisha wanachama wao wanafahamu
wajibu na haki zao katika Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF). Dkt.
Isaka ameyasema hayo katika hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya Sheria ya Fidia
kwa Wafanyakazi kwa viongozi na watendaji wa TUGHE taifa na mikoani iliyosomwa kwa niaba
yake na Mkurugenzi wa Utafiti na Tathmini SSRA, Joseph Mutashubilwa mjini
Morogoro Jumatatu Oktoba 1, 2018. “Kwa
kufanya hivi tutakuwa tunaepusha migogoro na tunadumisha mahusiano sehemu za
kazi hali itakayowavutia wawekezaji kuja nchini kwa wingi na hivyo kutimiza
dhamira ya Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wake Mhe. Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa viwanda.” Alsiema
Dkt. Isaka. Dkt.
Isaka pia aemwataka washiriki hao wa mafunzo kusambaza elimu watakayoipata kwa kuwatembelea
na kuwapa elimu wanachama wa chama hicho na kumtaka kila kiongozi/mtendaji
aliyeshiriki awe na mpango kazi utakaoonesha idadi ya wanachama alionao katika
eneo lake na namna atakavyowafikishia elimu hii ambayo ni muhimu kwao
kuifahamu.“Nina
imani kwa kufanya hivi tutakuwa tumewasaidia kwa kiasi kikubwa wanachama wetu
kuujua Mfuko, kazi zake na pia kufahamu nini wanapaswa kufanya baada ya kupata
matatizo wakati wakiwa wanatekeleza majukumu ya mwajiri.” Alifafanua. Akinukuu
kifungu cha 72 (4) cha Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi, Mkurugenzi Mkuu huyo wa
SSRA alisema kifungu hicho chan sheria kinatamka nafasi ya uwakilishi wa vyama
katika kamati za afya na usalama mahali pa kazi ambapo mwajiri anatakiwa
kutunza kumbukumbu hizo
na kamati inatakiwa kukagua ili kuona kama hilo linafanyika. Hayo yote ni
katika kuhakikisha kwamba upo ushirikishwaji wa baina viongozi/watendaji na
Serikali katika kulinda afya za wafanyakazi sehemu za kazi. Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Anselim Peter alisema, semina hiyo
ya mafunzo ni muendelezo wa hatua ya Mfuko kutoa elimu kwa makundi mbalimbali
ambayo ni wadau wa Mfuko na nia kubwa ni kuwajengea uelewa wa madhumuni ya
kuanzishwa kwa Mfuko, Sheria na jinsi Mfuko unavyofanya kazi. Alisema
katika kipindi cha miaka miwili tangu Mfuko uanze kutekeleza majukumu yake,
kumekuwepo na mafanikio makubwa ya kutimiza jukumu kuu la kuanzishwa kwa Mfuko la
kupokea madai na kulipa fidia na hadi sasa Mfuko tayari umekwishalipa fidia
zaidi ya shilingi bilioni 4.4. Naye
Katibu Mkuu wa TUGHE taifa, Bw. Hery Mkunda, yeye alisema, mafunzo hayo
yatawezesha kuongeza uelewa kuhusu wajibu wa mwajiri na haki kwa mfanyakazi
katika kuelewa sheria hiyo ya Fidia. “Washiriki
hawa ambao ni Makatibu wa Mikoa wa TUGHE ambao wao ndio husimamia haki na
maslahi ya wafanyakazi sehemu zao za kazi kuhakikisha wafanyakazi wanapata haki
zao kwa mujibu wa sharia watakuwa mabalozi wazuri katika kufikisha elimu hii kwa wanachama wetu.” Alisema.
Alisema kadisi siku zinavyokwenda, uelewa kuhusu shughuli za Mfuko umekuwa ukikua na kwamba hii imekuwa fursa nzuri kwa watendaji wa TUGHE ili waendelee kufuatilia na kuwafundisha wanachama wetu kuhusu haki zao hususan katika masuala haya ya Fidia kwa wafanyakazi.
Alisema TUGHE kwa sasa ina jumla ya wanachama 70,000 na lengo la chama ni kuongeza wanachama 10,000 kila mwaka kwa picha hiyo TUGHE ni "jeshi" kubwa na washiriki wa mafunzo ni makatibu wa mikoa ambao ndio wanashughulika moja kwa moja na wanachama kwa hivyo elimu itafika kwa walengwa.
"Matokeo ya semina hii ni hoja zilizojengwa na uongozi wa TUGHE tawi la WCF kwenye kkkao cha baraza la wafanyakazi kuonyesha umuhimu wa elimu hususan watendaji wanaoshughulika moja kwa moja kuwa na uelewa kuhusiana na shughuli za Mfuko.
"Tunawashukuru sana WCF kwa kuwezesha mafunzo haya na kimsingi watendajin wote kutoka TUGHE makao makuu na makatibu wa mikoa wamehudhuria." Alisema Bw.Mkunda.

No comments:
Post a Comment