Pages

Saturday, September 29, 2018

WAFANYAKAZI SHIRIKA LA UMEME TANESCO TANZANIA WATOA MSAADA WA SHUKA 150 KATIKA HOSPITALI TEULE YA RUFAA YA MKOA WA PWANI TUMBI


1 (12)
Kaimu meneja wa Shirika la umeme Mkoa wa Pwani (TANESCO) Selemani Mgwila kushoto akimkabidhi msaada wa mashuka 150  Mganga mkuu wa hospitali teule ya rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi Edward Wayi  ambao umetolewa na Cha chama cha ushirika cha wafanyakazi wa shirika la umeme  Tanzania.
2 (11)
Mganga mkuu wa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi Edward Wayi kushoto akisalimia na Kaimu meneja wa Shirika la umeme Tanesco Mkoa wa Pwani Selemani Mgwila mara baada ya halfa ya kukabidhiwa mashuka 150 kwa ajili ya wagonjwa.
3 (11)
Mjumbe wa bodi wa chama cha ushirika cha wafanyakazi wa shirika la umeme Tanzania (TANESCO) Mussa Chowo akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa halfa hiyo ya makabidhiano ya mashuka.
4 (10)
Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la umeme Tanzania (TANESCO)   wakiwa katika halfa hiyo  ya makabidhiano ya mashuka.
VICTOR MASANGU, PWANI

HOSPITALI  teule ya rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi kwa sasa inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo  upungufu wa mashuka,vifaa tiba, pamoja na uchakavu mkubwa wa
miundombinu wa majengo hivyo  kupelekea kupelekea usumbufu mkubwa kwa wagonjwa pindi wanapoitaji huduma kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Hayo yamebainishwa na Mganga mkuu wa hospitali hiyo  Edward Wayi wakati wa halfa fupi ya kukabidhiwa msaada wa mashuka 150 kutoka kwa chama cha ushirika cha wafanyakazi wa shirika la umeme  Tanzania (TANESCO) na kuhudhuliwa na wadau mbali mbali wa maendeleo katika sekta ya afya.
Wayi amesema kwamba kwa sasa katika hospitali hiyo ambayo ina jumla ya vitanda 254 hivyo bado kuna uhitaji mkubwa wa mashuka kwa ajili ya wagonjwa na kuongeza kuwa msaada huo walioupata kutoka Tanesco utaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kuboresha huduma kwa wagonjwa ambao wanakwenda kupatiwa matibabu.
Kwa upande wake Kaimu meneja wa Tanesco Mkoa wa Pwani Seleman Mgwila alisema kwamba lengo kubwa la kusaidia katika hospitali ya tumbi ni kutokana na utafiti ambao waliufanya na kubaini kuwepo kwa changamoto kubwa ya upungufu wa mashuka hivyo wameamua kutoa msaada huo wa mashuka 150 ambayo yatasaidia kupunguza kero ambayo waliyokuwa wakiipta wagonjwa hususan majeruhi wa ajali za barabarani.
“sisi kama Tanesco Saccos tulifanya utafiti tukaona kuna changamoto kubwa katika sekta ya afya hususan kwa wagonjwa kupata shida ya mashuka, hivyo sisi tukaona kuna umuhimu mkubwa wa kutoa msaada wa mashuka katika hospitali hii ya Rufaa ya Mkoa tumbi, kwa sasa tayari tumeshatoa mashuka kwa hospitali zote za Mkoa kwa nchi nzima,”alisema Mgwila.
Naye mjumbe wa bodi kutoka Tanasco Saccos Mussa Chowo alibainisha kuwa lengo lao kubwa ni kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya tano Dk, John Pombe Magufuli katika kuboresha sekta ya afya ambapo  amebainisha kuwa kwa sasa wameshatoa msaada wa  mashuka katika hospitali zote za Mkoa Tanzania nzima  ili kuisaidia jamii katika suala zima la  kupata huduma bora .

No comments:

Post a Comment