Waziri wa Nishati Dkt Medard
Kalemani (mbele) akiwa amefuatana na viongozi mbalimbali wa Serikali
kukagua hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa miundombinu wezeshi ya Mradi
wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Rufiji maarufu
kama Stieglers Gorge, Septemba 28, 2018.
Waziri wa Nishati Dkt Medard
Kalemani (kulia-mwenye miwani), akikagua zoezi la utandazaji mabomba ya
kupitisha umeme chini ya ardhi, katika eneo lenye viwanja vya ndege;
akiwa katika ziara kukagua hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa
miundombinu wezeshi ya Mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko
ya maji ya Mto Rufiji maarufu kama Stieglers Gorge, Septemba 28, 2018.
Waziri wa Nishati Dkt Medard
Kalemani (kushoto), akiwasalimia mafundi waliokuwa wakijenga Daraja,
akiwa katika ziara kukagua hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa
miundombinu wezeshi ya Mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko
ya maji ya Mto Rufiji maarufu kama Stieglers Gorge, Septemba 28, 2018.
Waziri wa Nishati Dkt Medard
Kalemani (mwenye shati la bluu-kulia) akizungumza na mafundi (kushoto),
wanaojenga barabara eneo la Rufiji, alipokuwa katika ziara kukagua hatua
iliyofikiwa katika ujenzi wa miundombinu wezeshi ya Mradi wa kuzalisha
umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Rufiji maarufu kama
Stieglers Gorge, Septemba 28, 2018.
Waziri wa Nishati Dkt Medard
Kalemani (mwenye shati la bluu-kushoto) akitoa maelekezo kwa taasisi
mbalimbali za Serikali zinazosimamia ujenzi wa miundombinu wezeshi ya
Mradi
wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Mto Rufiji
maarufu kama Stieglers Gorge. Waziri alikuwa katika ziara kukagua kazi
hiyo Septemba 28, 2018. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Japhet Hasunga.
Serikali yatoa siku 12 kukamilisha ujenzi wa miundombinu wezeshi mradi wa umeme wa mto rufiji
Na Veronica Simba – Rufiji
Serikali imeziagiza Taasisi zote
zenye jukumu la kujenga miundombinu wezeshi kwa ajili ya Mradi wa Kufua
Umeme wa Megawati 2100 kutokana na maporomoko ya Mto Rufiji, kuhakikisha
kazi hiyo inakamilika ifikapo Oktoba 10 mwaka huu.
Maelekezo hayo yalitolewa jana,
Septemba 28 na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiwa ameambatana
na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Japhet Hasunga, katika ziara ya
kukagua hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa miundombinu hiyo
itakayowezesha kuanza ujenzi wa Mradi husika.
“Tumeridhishwa na kazi
zinazofanyika ili kumwezesha Mkandarasi wa Mradi kuanza kazi yake,
lakini tunataka kazi zote za ujenzi wa miundombinu wezeshi zikamilike
ndani ya siku 12 kuanzia leo,” alisema.
Akifafanua zaidi, Waziri Kalemani
alisema ni matarajio ya Serikali kwamba kufikia tarehe iliyotolewa, kazi
zote zitakuwa zimekabidhiwa serikalini ili kumruhusu Mkandarasi
atakayepewa kazi ya kujenga Mradi husika, kuanza rasmi ujenzi.
Kufuatia maelekezo hayo, Waziri
Kalemani pia aliwaagiza wakandarasi na mafundi wanaojenga miundombinu
wezeshi ya Mradi huo, kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha kazi
kwa wakati.
Kalemani alimshukuru Naibu Waziri
Hasunga kwa kutoa maagizo ya kuhakikisha wanaotekeleza kazi husika
hawazuiliwi kufanya kazi usiku kwa kisingizio cha suala la usalama; na
kuagiza askari wa wanyamapori waongezwe ili kuimarisha ulinzi
utakaowawezesha wahusika kufanya kazi kama walivyoagizwa.
Awali, akielezea kazi za ujenzi wa
miundombinu wezeshi ya Mradi, zinazoendelea kutekelezwa; Waziri
Kalemani alisema ni pamoja na kuufikisha umeme katika eneo la ujenzi wa
Mradi.
“Tayari wameshafikisha umeme
kutoka Msamvu, wamekamilisha ujenzi wa vituo viwili vya kupooza umeme
vilivyopo Dakawa na Pangawe na wanaendelea kutandaza mabomba
yatakayopitisha umeme chini ya ardhi katika maeneo ya viwanja vya ndege
viwili. Aidha, kazi ya kuweka nguzo za zege na za miti inaendelea.”
Waziri alitaja kazi nyingine kuwa
ni ujenzi wa barabara zote kuelekea kwenye Mradi ikiwemo inayotoka Ubena
Zomozi, yenye umbali wa kilomita 178.4 pamoja na ya Kibiti – Lingungu
yenye umbali wa kilomita 210. Alisema kazi hii iko katika hatua nzuri.
Nyingine, ni ujenzi wa mitambo ya
maji pamoja na matenki makubwa mawili yenye uwezo wa kuhifadhi lita
22,500 hivyo kuweza kuhudumia wafanyakazi takribani 11,000; kazi ambayo
imekamilika.
Aidha, Waziri alisema kazi
nyingine ni ukarabati wa majengo ya nyumba za wafanyakazi pamoja na
ujenzi wa miundombinu ya mawasiliano kwa njia za simu, ambazo pia
zinaendelea na ziko katika hatua nzuri.
Akizungumzia utekelezaji wa Mradi
wenyewe wa kuzalisha umeme kutokana na maporomoko ya maji ya Mto Rufiji;
Waziri Kalemani alisema utahusisha kazi kuu tatu, ambazo ni pamoja na
kujenga Mtambo wa kuzalisha umeme wa megawati 2100.
Vilevile, alisema kuwa kazi
nyingine kubwa itahusisha ujenzi wa miundombinu ya kusafirisha umeme
kupitia njia mbili; kutoka eneo la Mradi hadi Chalinze, umbali wa
kilomita 178 wenye kilovoti 400 na kutoka eneo la Mradi hadi Kibiti
kupitia Lungungu, umbali wa kilomita 210 na wenye msongo wa kilovoti 400
pia.
Aidha, alieleza kazi nyingine kuwa
ni ujenzi wa Bwawa lenye eneo la kilomita za mraba 914 lenye uwezo wa
kuhifadhi maji kiasi cha mita za ujazo takribani bilioni 35.
Dkt Kalemani aliishukuru na
kuipongeza Serikali kwa kutoa fedha za ndani ili kutekeleza Mradi huo
mkubwa ambapo alisema mpango wa utekelezaji wake ulipangwa ufanyike
tangu miaka ya 1972 mpaka 1980 kwa awamu. “Naipongeza Serikali ya Awamu
ya Tano kwakuwa sasa tutaujenga kwa mkupuo.”
Ziara hiyo pia iliwahusisha
wabunge wa majimbo ya Rufiji (Omari Mchengelwa), Kibiti (Ally Ungando)
na Mafia (Mbaraka Dau), ambao wote walipongeza jitihada za Serikali
katika kuhakikisha Mradi huo unatekelezwa.
No comments:
Post a Comment