Katibu Mkuu Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu akiongea
wakati wa uzinduzi wa Siku ya Kimataifa ya Wazee leo jijini Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha ambaye
pia alikuwa mgeni rasmi Bw. Fabian Daqaro akiongea wakati wa ufunguzi wa
uzinduzi wa Siku ya Kimataifa ya Wazee leo jijini Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha wakwanza
kushoto Bw. Fabian Daqaro,Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu katikati na Kamishna wa
Ustawi wa Jamii Nchini Dkt. Naftali Ng’ondi wakikagua baadhai ya kazi za
ujasiliamali za kikundi cha wazee walipotembelea mabanda ya Wazee
kujionea shughuli zao.
Wazee wa Jiji la Arusha
walijitokeza kwa wingi kupima Afya wakati wa madhimisho ya Siku ya
kimataifa ya Wazee yanayoendelea Jijini Arusha.
Wazee 576,370 wamenufaika na
mpango wa kunusuru kaya masikini nchini tangu februari mwaka 2018 chini
ya TASAF na kati ya hao wanaume ni 217,947 na Wanawake 358,423 kwa
pande
zote za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya
anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema hayo wakati
wa uzinduzi wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee leo mjini
Arusha akitaja Siku hii kuwa inatukumbusha wajibu wetu katika kuwalinda,
kuwatetea na upatikanaji wa huduma bora kwa wazee.
Aidha Dkt. Jingu ameongeza kuwa
serikali inatekeleza Sera ya Taifa ya Afya ya mwaka 2007 kwa kuanzisha
Mpango wa Utambuzi wa Wazee katika Halmashauri na kuwapatia vitambulisho
vya matibabu bila malipo wazee wote wasiojiweza hapa Nchini.
Aidha pamoja na utekelezaji Sera
hiyo pia aserikali inaandaa Mkakati wa Kitaifa wa kutokomeza mauaji ya
wazee ambao utazinduliwa ifikapo Juni mwaka 2019 lakini pia serikali
itapitia Sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003 ili iendane na hali halisi
ya maisha ya Wazee.
‘’Kutokana na umuhimu wa uwepo wa
wazee katika familia, jamii na Taifa letu hatuna budi kuitumia siku hii
ya leo kuhamasishana, kuelimishina na kukumbushana wajibu wetu kwa wazee
wetu ili kuwawezesha kuishi maisha bora yenye staha’’. Aliongeza Dkt.
John Jingu.
Wakati huo huo Mkuu wa Wilaya ya
Arusha Bw. Fabian Daqaro ambaye amezindua rasmi maadhimisho ya Siku ya
Kimataifa ya Wazee ya Mwaka 2018 amesema wazee wote watanufaika na
msamaha wa kodi wa nyumba ambazo wanaishi lakini msamaha huo hautausika
na nyumba zote za biashara kama vile vyumba vya maduka au nyumba za
kupangisha.
‘’Naomba nieleweke vizuri kama
nyumba yako ni kuishi na haitumiki kwa biashara itapata msamaha wa kodi
lakini kama nyumba yako au nje ya nyumba yako yenye uzio ina sehemu za
kufanyia biashara itatozwa kodi ya serikali nendeni ofisi za Mapato
nakuweka takwimu zenu sahihi watawahudumia’’.Alisistiza Mkuu wa Wilaya
ya Arusha Bw. Fabian Daqaro.
Mkuu huyo wa Wilaya Arusha pia
amewataka watendaji wa Idara ya Afya Mkoani humo kuweka kumbukumbu
sahihi za Wazee mkoani humo ili wazee waendelee kutambuliwa ili
kuwawezesha wazee hao kupata huduma muhimu ikiwemo Afya,malazi chakuala,
ulinzi na hifadhi ya Jamii ya Uzeeni.
Siku ya Kimataifa ya Wazee Duniani
huadhimishwa hapa Nchini kila tarehe 1 mwezi wa kumi kufuatia Azimio la
Umoja wa Mataifa linalozitaka Nchi Wanachama kutenga Siku maalumu ya
kutafakari mchango wa wazee katika maendeleo ya jamii na Taifa kwa
ujumla
No comments:
Post a Comment