Pages

Sunday, September 30, 2018

IGP MSTAAFU AZIKWA DAR

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akiwa na IGP (mstaafu) Omar Mahita), Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi mstaafu, Jenerali Mwamunyange, Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Kamishna Jenerali Thobias Andengenye na Meja Jenerali Sharif Sheikh Othman aliyemwakilisha Mkuu wa Majeshi wakati wa mazishi ya IGP mstaafu marehemu Samwel Pundugu katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akitoa heshima baada ya kuweka shada la maua katika kaburi la IGP Mstaafu marehemu Samwel Pundugu katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 Maofisa wa Polisi wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa IGP Mstaafu marehemu Samwel Pundugu wakati wa mazishi yake katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam
 Askari Polisi wakishiriki kushusha jeneza lenye mwili wa IGP Mstaafu marehemu Samwel Pundugu kaburini wakati wa mazishi yake katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 Viongozi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na familia ya IGP Mstaafu marehemu Samwel Pundugu baada ya mazishi yake katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. (Picha na Jeshi la Polisi). 

No comments:

Post a Comment