Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma
Waziri wa Sheria na Katiba, Mhe. Profesa Palamagamba Kabudi
Picha ya pamoja
NA
IDARA YA HABARI-MAELEZO
JAJI
Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma, amewaasa wanasheria walio kwenye
utumishi wa umma kuzingatia misingi ya taaluma wakati wanapotekeleza majukumu
yao ya kila siku.
Kauli
hiyo ameitoa wakati akifungua mkutano wa pili wa wanasheria walio kwenye utumishi
wa umma unaofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Mipango, jijini
Dodoma.
“Mkiwa
maafisa wa Mahakama tunawatazamia kufanya kazi zenu kwa kuzingatia misingi ya
taaluma iliyowekwa kwa kuzingatia maadili, weledi, uwazi na usiri” alisisitiza
he Profesa Juma.
Profesa
Juma pia amewakumbusha wanasheria hao walio kwenye utumishi wa umma
kuhakikisha kuwa sheria wanazosimamia
zinalenga kuleta ustawi wa wananchi wanyonge na kuiwezesha serikali kutimiza
azma yake ya kifanya Tanzania iweze kufikia hadhi ya nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.
Vilevile,
wanasheria hao wa serikali wameaswa kuzingatia matumizi ya Teknolojia ya Habari
na Mawasiliano (TEHAMA) katika kutekeleza majukumu yao ili kuendana na kasi ya
mabadiliko ya karne ya 21.
Aliongeza
kuwa, wanasheria wanalo jukumu kubwa la kukidhi matarajio ya wananchi ikiwemo
Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025,
amani, usalama, umoja, utawala bora, na kujenga uchumi imara.
Kabla
ya Jaji Mkuu Profesa Juma, kuhutubia mkutano huo Waziri wa Katiba na Sheria,
Profesa Palagamba Kabudi alimshukuru
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kufanya
mabadiliko katika muundo wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambao
unategemewa kuleta ufanisi. Kwenye mabadiliko hayo yaliyoidhinishwa na Rais
Magufuli, yamesababisha kuanzishwa kwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Wakili
Mkuu wa Serikali.
Mkutano
huo wa siku mbili unawakutanisha wanasheria zaidi ya mia tisa kutoka Wizara,
Serikali za mitaa, Mashirika, Wakala na Idara mbalimbali za Serikali.
No comments:
Post a Comment