Na WAMJW- Mara
Takwimu
zinaonesha kuwa ukeketaji kwa mkoani Mara umepungua kutoka asilimia 72
mwaka 2008 mpaka 32 mwaka 2017 ikiwa ni jitihada za Serikali na wadau
katika kupambana na ukeketaji mkoani humo.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Faustine Ndugulile alipokuwa akizungumza na mangariba walioacha kazi hiyo, Wazee wa kimila wa koo 12 za makabila ya Tarime na wasichana na wanawake waliojikomboa na ukeketaji wilaya ya Tarime mkoani Mara.
Dkt. Ndugulile amesema kuwa suala la ukeketaji linatakiwa liangaliwa kwa jicho la tatu na kusisitiza kuachana na mila zisizofaa zinazochangia kutokea kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Ameongeza kuwa Wazee wa kimila wanatakiwa kuzingatia elimu ambayo ndio itakuwa msaada kwa Watoto wa kike na sio kuwakeketa na kuwafanya kitega uchumi kwa kuwaozesha katika umri mdogo.
"Suala la ukeketaji liwe historia na Mara bila ukeketaji inawezekana" alisisitiza Dkt. Ndugulile.
Nao Wazee wa kimila wilayani Tarime mkoani Mara wakiongozwa na Katibu wao Bw. Mwita Nyasibora wamemuhakikishia Naibu Waziri kuachana na vitendo vya ukeketaji ambavyo ni kinyume na haki za binadamu.
Pia Mangariba walioacha kukeketa wakiongozwa na Bi. Gati Mnyoro wamekiri kuacha na kuomba msaada wa mikopo kutoka Serikalini ili kujikita katika ujasiliamali ili kujikwamua kiuchumi.
Kwa upande wao wanawake na wasichana wakiongozwa na Bi. Spina Magesa wamewaasa wanawake na watoto wa kike kujitambua na kuwa kupambana na vitendo vya ukatili hasa ukeketaji.
Naye Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Tarime Bw. OchiengWayoga amemuhakikishia Naibu Waziri kuwasaidia mangariba walioacha na wanawake na Watoto waliokimbia ukeketaji kupata mikopo ya wanawake na vijana ili kujikwamua kiuchumi.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, JInsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na
Wazee 12 wa koo za makabila ya Tarime, Mangariba waliocha kazi hiyo na
wanawake na wasichana waliopambana wasifanyiwe ukeketaji.
Afisa
Maendeleo ya Jamii Bw. Ochieng Wayonge akielezea juhudi za Wilaya ya
Tarime katika kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa vitendo
vya ukeketaji kwa wanawake na watoto wa kike wakati wa mafunzo kwa
mangariba na wazee wa kimila kuhusu kuzuia ukeketaji wilayani Tarime.
Mwenyekiti
wa wazee kutoka koo 12 za makabila ya Tarime Bw. Mwita Nyasibora akitoa
ahadi mbele ya Naibu Waziri Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile kuacha kabisa vitendo vya
ukeketaji na kuhaidi kuwapa elimu watoto wa kike.
Mmoja
wa Mangariba waliocha kazi hiyo Gati Myoro akitoa ahadi mbele ya Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt.
Faustine Ndugulile kuacha kabisa vitendo vya ukeketaji na kuhaidi
kushirikiana na wazee wa kimila kuwapa elimu watoto wa kike.
No comments:
Post a Comment