Hellen Mlacky
WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame
Mbarawa amewataka wakandarasi walioshindwa kukamilisha miradi ya maji
kwa wakati, kutojaribu kuomba miradi mingine katika kipindi chake cha
uongozi.
Aidha, amewataka watendaji wake wizarani kubadilika pamoja na mamlaka za maji kufanya biashara na zijihudumie kwa kujilipia ankara za umeme na fedha zilizokuwa zikitoka wizarani zielekezwe kwenye miradi mingine ya maji ili kuwasaidia wananchi kupata maji.
Profesa Mbarawa aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana, katika Kongamano la Wadau wa Sekta ya maji lenye kaulimbiu 'Kuimarisha Ushirikiano kati ya Serikali na Sekta Binafsi katika kuendeleza Sekta ya Maji nchini'.
"Nimekaa wizara hii, wiki ya pili sasa na katika kipindi nilichokaa nimetembelea miradi minne mikubwa ikiwemo mradi wa Dar es Salaam, Chalinze na Kigoma. Miradi hii yote ina matatizo na ni ya muda mrefu na imechukua miaka mitano, lakini tatizo siyo pesa kwa kuwa yote inafadhiliwa na washirika wa maendeleo."amesema
"Mradi wa Kimara unaojengwa, mkandarasi wake ameacha kufanya kazi ingawa fedha zipo, Chalinze napo ni hivyo hivyo, pesa ipo, lakini mkandarasi amesimama, Kigoma kazi inafanyika, lakini si kwa spidi ambayo inatakiwa."
Profesa Mbarawa alisema yawezekana hayo yanatokea kwa sababu waliopata fursa ya kuchagua hawakuchagua vizuri kwa kutokujua kwamba hawana elimu, hawana uwezo au walifanya hivyo kwa maslahi yao binafsi.
"Kama wangechagua wakandarasi wenye viwango na wakaenda kufanya uhakiki wa miradi waliyoifanya hata kama ni Uganda au Namibia, naamini wananchi wa maeneo husika wangekuwa wameshapata maji. Hili ni tatizo na lazima wizara tulitatue, hatuwezi kumpa mkandarasi kwa sababu tunamjua au kwa sababu yupo karibu na Mbarawa au kiongozi fulani," alifafanua.
"Haiwezekani tukaendelea hivi, ninachowaeleza sasa ndivyo wizara itakavyokwenda... Tutawapa wakandarasi ambao wana viwango na tutawasimamia kuhakikisha kwamba wanafanya kazi kwa uadilifu na kwa muda tulioupanga kwa kuwa miradi ya maji ni rahisi sana kuijenga."
Alisema haiwezekani kuendelea kwa hali iliyopo na siyo sahihi na kusisitiza kwamba haiwezekani miradi ya miaka miwili inafanywa kwa miaka mitano hadi sita.
"Lazima tubadilike na huu ndo ujumbe wangu na nitausema kila mahali na ambaye hayupo tayari kubadilika mlango upo wazi tutampeleka wizara nyingine," alisema.
"Tumepewa jukumu la kuwahudumia Watanzania, lazima tuwahudumie na nyie wakandarasi mnaopata fursa hii lazima muwe wazalendo hata kama umetoka nchi nyingine. Nimeona kuna miradi midogo ya milioni 300 hadi 400, lakini mtu anachukua miaka mitatu hadi minne na nyie ndo makandarasi," alisema.
"Kuna wengine mnachukua hela mnazunguka halafu kazi haifanyiki, haiwezekani lazima tubadilike kama tumekupa mradi umechukua miaka minne na ni wa miaka miwili, usijaribu kuomba mradi mwingine nikiwepo, subiri nikiondoka utaomba, hatuwezi kuchukua mradi wa kuwapelekea wananchi miaka miwili sisi tunawapelekea miaka sita," alisema kwa ukali.
Kwa upande wa watendaji wa mamlaka za maji, alisema ni lazima kubadilika na kufanya biashara, na kutolea mfano mamlaka kama ya Kigoma imeshindwa kulipa umeme, pamoja na kwamba wana makusanyo ya kila siku.
"Hatuwezi kuwalipia, ukiuza maji unafanya biashara lazima upate hela. Mamlaka zina uwezo wa kujilipia umeme, hivyo wizara tusipeleke fedha, tuzitumie kuwapelekea wananchi maji. Mamlaka zote zisijekuomba fedha za kulipa umeme," alisema.
Alisema Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015 hadi 2020 imeainisha lengo la kuongeza upatikanaji wa maji ifikapo 2020 kutoka asilimia 72.25 hadi kufikia asilimia 85 kwa wananchi wanaoishi vijijini na kutoka asilimia 86 hadi asilima 95 kwa wananchi waishio mijini na kwamba wizara hiyo ndiyo imepewa jukumu la kusimamia lengo hilo.
"Ili kutimiza lengo hilo, wizara kwa kushirikiana na wadau wengine inatekeleza Awamu ya Pili ya Programu ya Kitaifa ya Maendeleo ya Sekta ya Maji ambayo ilianza 2017. Awamu ya kwanza ilianza Julai 2007 na kukamilika Juni 2016 ambapo shilingi trilioni 3.069 zilitumika," alieleza.
Alisema katika awamu ya pili inatarajiwa kutumika Sh trilioni 7.425 kwa ajili ya malipo ya kazi mbalimbali ambazo zitafanywa na sekta binafsi katika kupeleka huduma ya maji kwa wananchi.
Alisema baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza, wizara kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo walifanya tathmini ya ushiriki wa sekta binafsi kwenye utekelezaji wa progaramu hiyo na kubainisha changamoto mbalimbali moja, ikiwa ni uchache wa makampuni yanayoshiriki kwenye sekta ya maji, kazi kufanyika chini ya viwango stahili vya ubora na ucheleweshaji wa miradi ya ujenzi wa maji.
Alisema kongamano hilo pia litatoa fursa adhimu ya sekta binafsi kueleza kwa kina changamoto zinazowakabili na kutoa mapendekezo ya namna ya kushughulikia changamoto kwa lengo la kuongeza tija na hatimae kutimiza malengo ya sekta ya maji nchini.
Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Stella Manyanya amesema jukwaa hilo litakuwa chachu ya kuimarisha uhusiano ili kuleta mafanikio makubwa katika sekta ya maji na viwanda nchini.

No comments:
Post a Comment