Pages

Tuesday, July 31, 2018

MBUNGE JOSHUA NASSAR ASEMA KONGAMANO LILILOANDALIWA NA RAIS OBAMA LINAMANUFAA KWA VIONGOZI VIJANA BARANI AFRIKA

Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Joshua Nassar akizungumza jambo na Rais Mstaafu wa Marekani ,Barack Obama walipokutana nchini Afrika Kusini akiwa ni miongoni mwa Viongozi vijana 200  kutoka mataifa 44 ya Afrika waliochaguliwa kushiriki Programu ya  OBAMA AFRICA LEADERS PROGRAM.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Joshua Nassar kwa pamoja na Rais Mstaafu wa Marekani ,Barack Obama wakiwajibika kwa kufanya kazi za mikono katika kuboresha miundombinu ya shule ya Far North School iliyopo pembezoni mwa jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini.
Rais Mstaafu wa Marekani ,Barack Obama akipeana mikono na washiriki wengine wa Programu ya Viongozi wa Afrika mara baada ya kumaliza kazi za mikono katika shule hiyo.
Mbali na kushiriki kazi za mikono Rais Mstaafu wa Marekani,Barack Obama pia alipata nafasi ya kutoa mada katika kongamano lililowashirika viongozi vijana 200 kutoka mataifa 44 ya Africa.
Wengine waliowasilisha mada katika Kongamano hilo ni pamoja na Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa (UN) Koffi Annan ,Rais wa Kwanza Mwananmke Barani Afrika na Rais Mstaafu wa Liberia  ,Ellen Johnson Sirleaf
Pia Mjane wa Rais Mstaafu wa Afrika Kusini ,Mama Graca Machel alikuwa ni miongoni mwa viongoz walioshiriki kutoa mada kwa washiriki wa kongamano hilo.
Muanzilishi na Mmiliki wa Kampuni ya Celtel na muasisi wa Taasisi ya Mo Ibrahim Foundation inayoshiriki katika utoaji wa tuzo malumu kwa viongozi mbalimbali wa bara la Africa waliofanya vizuri,Mo Ibrahim pia alishiriki katika kutoa mada katka Kongamano hilo.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar akiwa na vijana wengine wa Kitanzania wakishikilia Bendera ya Taifa wakati wa Kongamano hilo lililoandaliwa na Taasisi ya Obama Foundation.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassar akiwa na Waziri wa Viwanda ,Biashara na uwekezaji Botswana Bogolo Kenewendo .
Mbunge wa Jimbo la Arumerua Mashariki ,Joshua Nassar akiwa na Waziri wa Ubunifu na Mafunzo ya Ufundi nchini Cape Verde ,Pedro Lopez.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar akiwa na mmoja wa Familia ya Mmiliki wa Klabu ya Mancheter United ,Malcolm Glazer,walipokutana wakati wa Kongamano

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.
MBUNGE wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar amesema ushiriki wa Viongozi vijana wa Kiafrika Katika Kongamano lililoandaliwa na Taasisi ya Rais Mstaafu wa Marekani ,Barack Obama ,Obama  Foundation ni chachu kwa viongozi walioko madarakani kuendelea kuwamini kwa kuwapa nafasi za ju za uongozi .
Nassar ametoa kauli hiyo zikiwa zimepita siku chache tangu ashiriki Kongamano lililoandaliwa na taasisi ya Obama Foundation na kuwashikisha vijana 200 kutoka mataifa 44 barani Afrika  wanaofanya kazi serikalini ,asasi za kiraia na sekta binafsi ambao walikutana kwa muda wa siku tan katika jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini.
Amesema katika Kongamano hilo kama vijana wamejifunza mambo mengi ambayo kwa kiasi kikubwa yatachangia kujitokeza kwa vijana wengi zaidi katika kuwania nafasi mbalimbali za uongozi watakaosaidia kuleta mabadiloko chanya katika bara la Africa.
Katika kongamano hilo lililoenda sambamba na sherehe za kilele cha kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa muasisi wa taifa la Afrika Kusini ,Nelson Mandela,vijana nane kutoka Tanzania walichaguliwa kuiwakilisha nchi ya Tanzania.
Miongoni mwa Viongozi na watu Mashuhuri walioshiriki katika utoaji wa mada katika kongamano hilo ni pamoja na Rais Mstaafu wa Marekani ,Barack Obama,Rais Mstaafu wa Liberia,Ellen Johnson Sirleaf,  Katibu Mkuu Mstaafu wa UN,Koffi Annan na Mmiliki wa Kampuni ya Celtel na Muasisi wa taasisi ya Mo Ibrahimu ,Bw Mo Ibrahim.
Wengine ni Mke wa Rais Mstaafu wa Afrika Kusini,Mama Graca Machel,Mfanyabiashara Tajiri,Aliko Dangote, Waziri (mdogo) wa Viwanda ,Biashara na Uwekezaji Botswana ,Bogolo Kenewendo,Muandishi wa filamu maarufu zaidi Duniani ya Black Panther ,Ryan Coogler Lakhdar Brahimi ,Trevor Manuel  na wengine wengi.

No comments:

Post a Comment