Pages

Tuesday, July 31, 2018

DK. KALEMANI AZINDUA UMEME USIKU VIJIJINI


 Diwani wa Viti Maalumu, Grace Kubilima (CCM), ambaye pia ni mkazi wa Kijiji cha Ihanga, akimshukuru Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, baada ya kuzindua umeme jana usiku katika kijiji hicho.
 Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ihanga Wilayani Chato usiku wa jana baada ya kuzindua umeme
Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ihanga Wilayani Chato usiku wa jana baada ya kuzindua umeme

NA MWANDISHI WETU, CHATO
WAZIRI wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, ameendelea na ziara yake vijijini y kukagua miradi ya umeme REA III inayoendelea huku akilazimika kuzindua umeme usiku.
Amesema amelazimika kufanya uzinduzi huo usiku ili kutoa maana halisi ya uwepo wa mwanga wa umeme kwa wananchi ili nao waone hali halisi kuliko ya jinsi raha ya umeme ilivyo.
Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ihanga Wilayani Chato, alisema kuwa Serikali pamoja na watalaamu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco)  kwa kushirikiana na REA wamekuwa wakifanyakazi usiku na mchana ili kuhakikisha  kazi ya uunganishaji umeme inafanyika kwa maslahi ya wananchi na kuvutia wawekezaji hasa wa viwanda.
“Ninawashukuru sana wananchi kwani watu wengi wana shauku ya umeme na kila unapokwenda ukiwaambia leo ninakuja kuwaunganishia umeme wako tayar kusubiri mpaka usiku, niwapongeze wananchi kwa kweli walikuwa na shauku kubwa na leo wamepata furaha.
“Na mimi kama mbunge wao bahati nzuri ni Waziri wa Nishati ilikuwa ni lazima kuwatembelea hata kama ingekuwa usiku. Lakini pia huu ni mwanga ili udhibitishe kama ni mwanga ni vizuri ukawasha usiku ikaonekana kuwa kweli hii ni taa. Nadhani walitaka wajiridhishe na wameshuhudia kwa sababu tumewasha usiku na kwangu nitatembea usiku na mchana kuwatumikia Watanzania ili mradi nitahakikisha  wanapata maendeleo,” alisea Dk. Kalemani
Akizungumzia suala la nguzo za umeme, Dk. Kalemani, alisema kuwa kwa sasa nchi ina nguzo nyingi kwani kwa mwezi huingizwa zaidi ya nguzo 118,000  na si 2000 kama ilivyokuwa nyuma.
Alisema kuna kampuni 21 za zinatosambaza nguzo nchini.
“Zamani tulikuwa na wasambazaji nguzo watano lakini kwa sasa tuna kampni 21 hiyo imetokana na kusitisha uagizaji wa nguzo kutoka nje ya nchi ambazo zilikuwa na gharama kubwa sana kwa Shirika letu la umeme Tanesco lakini hata wakandarasi. Sasa hivi nguzo wazalishaji wa nguzo ni wengi kwani hata gharama zimeshuka na pia suala la transfoma si changamoto.
“Mradi unapoanza wanaleta nguzo kutokana na mahitaji kutokana na eneo husika leo wameanza na nguzo chache lakini kadri ya wananchi wanavyojiandisha magari huleta nguzo nyingi zaidi ili kuweza kutoa huduma ya kuunganisha umeme. Na wiki ijayo wataleta nguzo nyingine 200 ombi langu wananchi wajiandikisha na kulipia ili nguzo ziendele kuwa nyingi.
“Watanzania wana shauku ya kulipia umeme sasa Serikali imekuja na mpango wezeshi badala ya wananchi kwenda Tanesco sasa litaanzishwa dawati dogo katika maeneo ya vijiji ili kuwapunguzia gharama za kutembea umbali mrefu.
“Pia wananchi wanaweza kulipia kidogo kidogo na pindi wanapofikisha Shilingi 27,000 ataunganishiwa huduma ya umeme,” alisema Dk. Kalemani

No comments:

Post a Comment