Kikundi
cha Ngoma cha Sange kikitumbuiza ngoma ya Ling'oma wakati wa
kumkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye
kijiji cha Sange wilayani Ileje ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya
kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Songwe.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akipata maelezo ya shamba la Misitu kutoka kwa Mkurugenzi wa
Mipango-Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Bw. Mohamed Kilongo kwenye
uzinduzi wa shamba la misitu la Serikali la Iyondo-Mswima wilayani Ileje
ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo
mkano Songwe.
NA
OMR, ILEJE
MAKAMU
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo
amezindua shamba la miti katika hifadhi ya Misitu Iyondo Mswima lililopo
Katengele wilayani Ileje mkoani Songwe ikiwa ni siku ya nne ya ziara yake ya
kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Songwe.
Shamba
hilo lililo chini ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ni moja kati ya
mashamba mapya yakiwemo Biharamulo (Chato Geita), Buhigwe (Kigoma) na Mpepo
(Mbinga, Ruvuma).
Akisoma
taarifa ya Shamba hilo kwa Makamu wa Rais, Mkurugenzi wa Mipango –Wakala wa
Misitu Tanzania Bw. Mohamed Kilongo amesema kuwa mpaka shamba la miti la Iyondo
Mswima limeweza kutoa ajira kwa wananchi 400 katika msimu wa kupanda miti, pia
shamba limetoa ajira zingine 200 wakati huu wa maandalizi ya bustani ya miti,
hekta 201 zimepandwa miti kama sehemu ya upanuzi wa mashamba ya miti ya
Serikali ambapo bustani yenye jumla ya miche 430,000 kwa ajili ya upandaji miti
wa mwaka 2018/2019.
Akizungumza
na wananchi wa kijiji cha Katengele ambapo shamba la misitu la Serikali Iyondo
Mswima limezinduliwa, Makamu wa Rais
amewataka wananchi hao kutunza na kuyalinda mazingira kwa kupanda miti kwa
wingi ambapo kila mwaka wananchi watapewa miche 50,000 na Wakala wa Huduma za
Misitu wa Serikali.
Makamu
wa Rais pia alipata nafasi ya kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Sange ambapo
aliwaambia wananchi wa kijiji hicho kuwa Mungu amewapa rasilimali nzuri sana
hivyo hawana budi kuyatunza.
Makamu
wa Rais amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ileje kuhakikisha Maafisa Ugani wanashuka
kwa wananchi na kutoa ushauri namna ya kufanya shughuli za kilimo vizuri.
Makamu
wa Rais amesema Serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni 1.5 katika bajeti
mwaka huu iliyopita kwa ajili ya kujenga hospitali ya wilaya ya Ileje.
Makamu
wa Rais amesema mkoa wa Songwe utapata watumishi 270 katika Sekta ya Afya, na
kwenye sekta ya elimu, walimu wengi wameajiriwa mwaka huu ambapo Songwe nayo
itapata walimu wapya.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na wananchi wa kijiji cha Katengele mara baada ya kuzindua
shamba la misitu la Serikali la Iyondo-Mswima wilayani Ileje ikiwa siku
ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkano
Songwe.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akipata maelezo ya shamba la Misitu kutoka kwa Mkurugenzi wa
Mipango-Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Bw. Mohamed Kilongo kwenye
uzinduzi wa shamba la misitu la Serikali la Iyondo-Mswima wilayani Ileje
ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo
mkano Songwe.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na wananchi wa kijiji cha Katengele mara baada ya kuzindua
shamba la misitu la Serikali la Iyondo-Mswima wilayani Ileje ikiwa siku
ya nne ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkano
Songwe.
Makamu wa Rais akikata utepe kama ishara ya kuzindua shamba la miti katika hifadhi ya Misitu Iyondo
Mswima lililopo Katengele wilayani Ileje mkoani Songwe
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akisalimiana na Mbuge wa Jimbo la Ileje Mhe. Janeth Mbene mara baada ya
kuwasili kwenye uzinduzi wa shamba la misitu la Serikali la
Iyondo-Mswima wilayani Ileje ikiwa siku ya nne ya ziara yake ya
kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkano Songwe.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akihutubia wakazi wa kijiji cha Sange wilayani Ileje ikiwa siku ya nne
ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkano Songwe.(PICHA
NA OMR)

No comments:
Post a Comment