Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama
Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Erasto Sima, akihutubia wakati akimnadi
Mgombea Udiwani wa Kata ya Unyambwa, Abdulaziz Hamisi Labu (kushoto),
katika mkutano wa kampeni uliofanyika jana katika kata hiyo mkoani
Singida. Uchaguzi mdogo utafanyika katika kata hiyo tarehe 12 mwezi ujao
baada ya diwani wa awali kufariki dunia.
Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu, akimnadi mgombea huyo.
Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Singida Mjini, Lusia Andrew Mwiru akimdani mgombea huyo.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo wa kampeni.
Madiwani wa wilaya hiyo wakimuombea kura mwenzao kwa wananchi.
Wananchi wakifuatilia kwa makini mkutano huo wa kampeni.
Taswira ya meza kuu kwenye mkutano huo.
Mke wa mgombea udiwani huyo, Farida Iddi akimuombea kura mume wake.
Viongozi mbalimbali wa CCM na wanachama
wao wakiserebuka katika mkutano huo wakati wa kumkaribisha Katibu wa
Jumuiya ya Wazazi Taifa, Erasto Sima ili kuhutubia.
Mbunge wa Singida
Magharibi, Elibariki Kingu (katikati), akiteta jambo na Mwenyekiti wa
CCM Wilaya ya Singida Mjini, Lusia Mwiru. Kulia ni Mkuu wa Wilaya
mstaafu wa Wilaya ya Nchemba.
Viongozi mbalimbali wa Kata hiyo wakitambulishwa.
Mgombea Udiwani wa Kata hiyo, Abdulaziz Labu akijinadi.
Mbunge wa Singida
Magharibi, Elibariki Kingu, akicheza sanjari na Katibu wa Jumuiya ya
Wazazi Taifa, Erasto Sima baada ya kwisha mkutano huo wa kampeni.
Makada wa CCM wakiserebuka na viongozi wao baada ya mkutano huo wa kampeni kumalizika.
Na Dotto Mwaibale, Singida
KATIBU wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Taifa, Erasto Sima amewaomba wanaccm wa Kata ya
Unyambwa mkoani Singida kuhakikisha wanamchagua Abdulazziz Labu kuwa
Diwani wa Kata hiyo.
Sima ambaye alikuwa ni mgeni rasmi
alitoa ombi hilo wakati akihutubia kwenye mkutano wa ufunguzi wa kampeni
ya mgombea udiwani huyo uliofanyika jana katika kata hiyo.
"Ndugu zangu wanaccm wenzangu msituangushe mchagueni Labu ili awaletee maendeleo katika kata yenu" alisema Sima.
Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki
Kingu akihutubia kwenye mkutano huo alisema atashirikiana na diwani huyo
kuhakikisha changamoto ya maji iliyopo katika kata hiyo inapatiwa
ufumbuzi.
Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Singida
Mjini Lusia Mwiru aliwaomba wananchi na makada wa CCM wa Kata hiyo
tarehe 12 mwezi ujao kumchagua Labu kuwa diwani ili ashirikiane na
serikali inayoongozwa na Rais Dk.John Pombe Magufuli kuwaletea
maendeleo.
Kwa upande wake mgombea huyo aliomba
kura kwa kuwaambia wananchi hao kuwa akichaguliwa atawafanyia mambo
makubwa ya kuwaletea maendeleo akianzia pale alipoishia mtangulizi wake
ambaye amefariki.
No comments:
Post a Comment