Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea
gawio toka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za
Taifa (TANAPA) Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara katika
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es
salaam Jumatatu Julai 23, 2018
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo Julai 23 2018,
amepokea mfano wa hundi zenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 723.61,
ikiwa ni gawio kutoka Mashirika, Taasisi na Kampuni 40 ambazo Serikali ina hisa.
Makabidhiano
hayo yamefanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere(JNICC)
jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
kabla ya kumkaribisha Rais Magufuli,
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango alisema, fedha hizo ni asilimia
15 ya ,mapato ghafi kutoka, Taasisi, Mashirika ya Umma na Makampuni na
kuchangia kwenye mfuko mkuu wa serikali.
Akizunguzma
kwenye hafla hiyo, Rais Magufuli alipongeza Taaisi, Mashirika na Kampuni ambazo
zimefanikiwa kuwasilisha gawiwo la serikali.
Hata
hivyo Rais alisema Serikali imewekeza zaidi ya Shilingi Trilioni 49 na kwamba
haiwezekani ipate gawio la Shilinhgi Bilioni 736, hivyo amemuagiza Msajili wa
Hazina ambaye ndiye anayesimamia taasisi, Mashirika na Makampuni yenye ubia na
Serikali kuhakikisha wanatoa gawiwo.
na
yatakayoshindwa uongozi wake ubadilishwe au yafutwe. “Hapa pesa kwanza
halipendwi shirika inapendwa pesa” Alisema. Rais Mahifuli.
Alisema,
zipo njia nyingi za kukusanya mapato ya serikali na mojawapo ni hii ya kupoeka
gawiwo kutoka Mashirika, Taasisi na Makampuni ambayo Serikali ina hisa zake.
“Huwezi
kuendesha nchi kwa kutegemea makusanyo ya kodi pekee, na tulipofanya utafiti
kwanini serikali haipati mapato yake kutoka kwenye uwekezaji iliyoufanya kwenye
mashirika, Taasisi na Makampuni, tulibaini kuwa ni uongozi mbovu, na kukithiri
kwa rushwa.” Alibainisha Rais Magufuli.
Akizungumza
kabla ya kumkaribisha Rais Magufuli, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip
Mpango alisema, “Makampuni, Taasisi na Mashirika ambayo hayajawasilisha gawio,
wajitathmini, ikiwa ni pamoja na wawekezaji ambapo bado hawajatimiza malipo
wafanye hivyo mara moja.” Alisema Dkt. Mpango
Alitaja
Mashirika, Taasisi ambazo zimevuka lengo la ukusanyaji wa mapato waliojiwekea kuwa
ni pamoja na Ngorongoro Conservation Area, ambao walilenga kutoa Bilioni 13.24 lakini
wakaongeza hadi Shilingi Bilioni 22.35 na Taasisi nyingine ni
Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), amabayo lengo ilikuwa ni kupeleka gawiwo la
Shilingi Bilioni 30.69, lakini wamepeleka Shilingi Bilioni 59.89 wakati TANAPA
walijiwekea lengo la kuleta Shilingi Bilioni 30.77 lakini wamepeleka Shilingi
Bilioni 34.74
Hata
hivyo bado kuna mashirika 158 bado yanategemea ruzuku kutoka serikalini huku
makampuni 48 yameshindwa kutoa gawio
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea
gawio toka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya TIPER Profesa Abdulkarim
Mruma katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere
jijini Dar es salaam Jumatatu Julai 23, 2018
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea
gawio toka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Maendeleo ya Biashara
(TANTRADE) akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade Bw. Edwin Rutageruka
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea
gawio toka kwa Mfuko wa Misitu Tanzania akiwa na Katibu Dkt. Tuli Salum
Msuya katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini
Dar es salaam Jumatatu Julai 23, 2018
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea
gawio toka kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na (EWURA) Maji
Profesa Jamidu Kamika akiwa na Kaimu Mkurugenzi mkuu wa EWURA Bw.
Nzinyangwa Mchani katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu
Nyerere jijini Dar es salaam Jumatatu Julai 23, 2018
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea
gawio toka kwa Mwenyekliti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA)
Profesa Rutasitara akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw. Hamza
Johari katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere
jijini Dar es salaam Jumatatu Julai 23, 2018
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea
gawio toka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Chakula na
Dawa (TFDA) Balozi Ben Moses akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa TFDA Bi. Agnes
Kijo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere
jijini Dar es salaam Jumatatu Julai 23, 2018
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea
gawio toka kwa Mwenyekiti wa Shirika la Viwango (TBS) Prof. Makenya
Abraham Honoratus Maboko akiwa na Mkuruigenzi wa TBS Profesa Egird
Mubofu katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere
jijini Dar es salaam Jumatatu Julai 23, 2018
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea
gawio toka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Bandari Profesa Ignas
Rubaratuka aliye pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Mhandisi
Deusdedit Kakoko katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu
Nyerere jijini Dar es salaam Jumatatu Julai 23, 2018
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea
gawio toka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la
Bonde la Ngorongoro Profesa Abiud Lucas Kaswamila akiwa a Mhifadhi Mkuu
wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro Dkt. Freddy Manongi katika
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es
salaam Jumatatu Julai 23, 2018
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na meza kuu
wakipata picha ta pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kudumua ya Bunge ya
Uwekezaji wa Mtaji wa Umma baada ya kupokea magawio kutoka katika
taasisi, mashirika na Makampuni ya Umma katika Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam Jumatatu Julai 23,
2018,(PICHA NA IKULU)












No comments:
Post a Comment