Pages

Thursday, May 3, 2018

Waziri wa Nishati Ashiriki Mkutano wa Japan- Africa Public Private Economic Forum Nchini Afrika Kusini


south moja
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (wa Tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wengine wa Mkutano  wa Kimataifa wa Japan -Africa Public Private Economic Forum unaofanyika katika Jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini.
southmbili
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (wa nne kushoto) akiwa akiwa katika  Mkutano wa Kimataifa wa Japan -Africa Public Private Economic Forum unaofanyika katika Jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini.Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji,  Mhandisi Stella Manyanya.
……………….
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ameshiriki Mkutano  wa Kimataifa wa Japan -Africa Public Private Economic Forum katika Jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini  ambao pamoja na masuala mengine utajadili suala la uwekezaji katika Sekta ya Nishati.
Katika Mkutano huo unaofanyika tarehe 3-4, Mei, 2018, Dkt Kalemani  ameambatana na Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji,  Mhandisi Stella Manyanya na maafisa kutoka Sekta mbalimbali nchini.
Katika Mkutano huo, kampuni mbalimbali kutoka nchini Japan  zimeonesha nia ya kuwekeza nchini katika viwanda mbalimbali ikiwemo vya kutengeneza magari aina ya Toyota.
Mkutano huo umehudhuriwa na kampuni kubwa  zaidi ya 200 kutoka nchini Japan, ambapo kampuni hizo  zitaonesha teknolojia za kisasa zinazotumika katika kutengeneza vifaa mbalimbali vya kielektroniki na mitambo ya kuzalisha umeme.

No comments:

Post a Comment