Dkt. Olivia Rusizoka ambaye
amemwakilisha Mkurugenzi wa Huduma za Tiba katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH), Dkt. Hedwiga Swai akifunga mafunzo ya siku tano
yaliowashirikisha wataalamu wa afya wa Magomjwa ya Dharura na Ajali
kutoka manispaa tano za Jiji la Dar es Salaam ambayo yaliandaliwa na
Muhimbili, EMAT na MUHAS . Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya
Dharura na Ajali katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga
na Dkt. Upendo George wakiwa kwenye mkutano wa kufunga mafunzo hayo.
Wataalamu wa kutoa huduma za
magonjwa ya Dharura na Ajali wakiwa kwenye mkutano wa mafunzo ya
nadharia na vitendo ambayo yamefungwa na Dkt. Rusizoka aliyemuwakilisha
Mkurugenzi wa Tiba, Dkt. Hedwigwa Swai.
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya
Dharura na Ajali wa Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga akisisitiza madhumuni
na umuhimu wa kuendesha mafunzo hayo. Kulia ni Dkt. Rusizoka na Dkt.
Upendo.
Wataalamu wanaotoa huduma ya magonjwa ya Dharura na Ajali wakiwa kwenye mafunzo ya vitendo.
Mmoja wa wataalamu wa kutoa huduma za Magonjwa ya Dharura na Ajali, Fatma Chichiri akipokea cheti kutoka kwa Dkt. Rusizoka.
Mmoja wa wataalamu wa huduma hizo, Buheri Kiberiti akikabidhiwa cheti baada ya kukamilika kwa mafunzo hayo.
Mtaalamu wa kutoa huduma za
magonjwa ya Dharura na Ajali, Tuma Kanyumbu akipokea cheti kutoka kwa
Dkt. Rusizoka. Kushoto ni Msimamizi wa mafunzo hayo, Dkt. Patrick
Shayo, Dkt. Juma Mfinanga, Dkt. Rusizoka na Dkt. Upendo Geonge.
Wataalamu wa kutoa huduma za
magonjwa ya Dharura na Ajali wakiwa kwenye picha ya pamoja na
wakufunzi wao baada ya mafunzo kufungwa na Dkt. Rusizoka.
JOHN STEPHEN, Hospitali ya Taifa Muhimbili
…………………..
Wataalamu
Bingwa wa Huduma ya Tiba ya Dharura na Ajali wa Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH), Chuo Kikuu cha Sayansi ya Afya na Tiba
Shirikishi(MUHAS)kwa kushirikian na
Chama cha Wataalamu wa Magonjwa ya
Dharura na Ajali Tanzania (EMAT) wameendesha mafunzo ya awali kwa watoa
huduma kuhusu ya magonjwa ya dharura na ajali.
Mafunzo
hayo ya siku tano yalifanyika kwa watumishi 16 wanaotoka katika
hospitali za rufaa katika Manispaa tano za Mkoa wa Dar es Salaam,
wakiwamo waaguzi saba, afisa wauguzi wanne, tabibu wasaidizi watatu,
Madaktari wasaidizi watatu na daktari mmoja.
Mafunzo hayo yalilenga watoa huduma ambao wamekuwa wakifanya kazi kwenye magari ya
wagonjwa
(Ambulance) katika Mkoa wa Dar es salaam ikiwa ni maandalizi ya kozi ya
wiki sita inayotegemewa kufundishwa na MUHAS kwa kushirikiana na Idara
ya Magonjwa ya Tiba ya Dharura na Ajali ya Muhimbili kwa watoa huduma
wa ambulance Tanzania.
Katika
mafunzo hayo, wanafunzi walifundishwa mafunzo ya nadharia na vitendo
kwa baadhi ya mada ambazo zinatarajiwa kutolewa kwenye kozi hiyo ili
kuona kama mtaala huo uko tayari na unajitosheleza kuanza kutumika kwa
walengwa kabla ya kozi rasmi ya wiki sita kuanza.
Mada
zilizofundishwa ni; Basic ambulance safety, Documentation and
Communications, Pre hospital trauma, Obstretics emergencies, Patient
movement. Mwisho wa mafunzo hayo wanafunzi walipewa vyeti vya ushiriki
wa mafunzo hayo
No comments:
Post a Comment