Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Freeman Mbowe, na viongozi wengine
waandamizi wa chama hicho, wamefutiwa dhamana katika Kituo Kikuu cha
Polisi Dar walipokuwa wameripoti kwa ajili ya kuendelea kuhojiwa na
Naibu Mkuu wa Upelelezi wa Kanda (ZCO) na kupelekwa katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu kusomewa mashitaka yanayowakabili.
Mbowe na viongozi wenzake ambao ni
Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt. Vincent Mashinji; Naibu Katibu Mkuu
Bara, John Mnyika; Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu; Mjumbe wa
Kamati Kuu ya chama, Peter Msigwa na Ester Matiko, wamefikishwa
Mahakamani hapo kwa tuhuma za kuendesha maandamano kinyume na taratibu.
Maandamano yanayodaiwa
kuendeshwa na viongozi hao ni yale yaliyofanyika Februari 16, mwaka huu
na kusababisha polisi kuwatawanya waandamanaji na kupelekea kifo cha
mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT), Akwilina Akwilini
maeneo ya Kinondoni jijini Dar.
No comments:
Post a Comment