Pages

Tuesday, March 27, 2018

KAMATI YA BUNGE YA UTAWALA YAENDELEA NA VIKAO VYAKE MJINI DODOMA


IMGL6410
Makamu Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Mwanne Mchemba akizungumza na Wajumbe wa kamati hiyo pamoja na viongozi wakuu kutoka Mkoa wa Simiyu (hawapo kwenye picha) walioongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa kupokea na kujadili Taarifa kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2017/2018 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019. Kulia ni katibu kamati wa kamati hiyo, Ndg. Victor Leonard
IMGL6337
Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Saada Mkuya akizungumza na Wajumbe wa kamati hiyo pamoja na viongozi wakuu kutoka Mkoa wa Simiyu (hawapo kwenye picha) walioongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa kupokea na kujadili Taarifa kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2017/2018 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 katika kikao kilichofanyika leo ukumbi wa Pius Msekwa Mjini Dodoma. Kushoto ni Mjumbe wa kamati, Mhe. Lucia Mlowe
IMGL6181
Baadhi ya Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakifuatilia mazungumzo wakati wa kupokea na kujadili Taarifa kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2017/2018 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019. Kutoka kushoto ni Mhe. Lucia Mlowe, Mhe. Saada Mkuya, Mhe. Mwantum Haji na Mhe. George Lubeleje
IMGL6431
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakati wa kupokea na kujadili Taarifa kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2017/2018 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019. Kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa huo, Mhe. Jumanne Sagini
 (PICHA NA OFISI YA BUNGE

No comments:

Post a Comment