Mwanasheria Mkuu Dk. Adelardus
Kilangi akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe Wilbroad
Slaa walipokutana nje ya Jengo ambalo lina Ofisi ya Mwanasheria Mkuu
wa Serikali na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
. Mwanasheria Mkuu alikuwa akimsubiri kumpokea mgeni wake Jaji Mkuu wa
Gambia Mhe. Hassan Jallow ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali
akiagana na Mgeni wake Jaji Mkuu wa Gambia Mhe. Hassan Bubacar Jallow
mara baada ya mazungumzo yao. Jaji Mkuu Jallow alisoma sheria Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam (1970-1973) na pia amewaji kuwa Mwendesha
Mashtaka wa iliyokuwa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya
Rwanda ( ICTR) (2003-2015).
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk.
Adelardus Kilangi akibadilishana mawazo na Jaji Mkuu wa Gambia Mhe.
Hassan Bubacar Jallow, leo Ofisi kwa Mwanasheria Mkuu. Jaji Mkuu yupo
hapa nchini kwa ziara ya kikazi yenye madhumuni ya kujifunza uboreshaji
wa sekta ya sheria na utoaji haki hapa nchini. Baadhi ya mambo
waliyobadilishana mawazo ni pamoja na uwezeshwaji kwa wanasheria wa
Serikali na watumishi wengine katika sekta ya sheria kimaslahi na
kimafunzo.
………………………………………………………………………
Na Mwandishi Maalum
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk.
Adelardus Kilangi, leo (Alhamisi) amekutana na kuwa na mazungumzo na
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Gambia Mhe. Hassan Bubacar Jallow.
Jaji Mkuu wa Gambia, yupo hapa
nchini kwa ziara ya kikazi ya kujifunza na kujipatia
uzoefu kuhusu
mfumo wa utoaji haki hapa nchini pamoja na maboresho mbalimbali
yakiwamo ya maslahi ya watumishi yanayoendelea katika Mahakama ya
Tanzania na Taasisi nyingine za Sheria na utoaji haki.
Jaji Mkuu Jallow amemueleza
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Adelardus Kilangi kwamba, Gambia,
baada ya mabadiliko ya Serikali yaliyofanyika mwaka jana nchini humo,
ipo katika mchakato wa kuifanyia mabadiliko na maboresho sekta ya
sheria nchini humo.
“Nimekuja kwa ziara ya kikazi kwa
madhumuni ya kujifunza kutoka Tanzania namna gani na sisi (Gambia)
tutakavyoweza kuboresha na kuifanyia mageuzi makubwa sekta yetu ya
Sheria na mfumo mzima wa utoaji wa haki”.
Akabainisha kwamba, anafahamu,
namna gani Mahakama ya Tanzania imeweza, kwa kushirikiana na
Serikali na Wadau wa Maendeleleo hususani Benki ya Dunia kufanya
mageuzi na maboresha makubwa katika mfumo wa utoaji haki.
“Ningependa kujifunza mbinu
ambazo Mahakama iliweza kuzitumia kuivutia Benki ya Dunia hata ikawa
mdau wake muhimu katika maboresha yanayoendelea hivi sasa. Na pia
nitumie fursa hii kubadilishana mawazo pamona na wewe Mwanasheria Mkuu
na nikupongeze kwa kuteuliwa kwako.” akaeleza Jaji Mkuu.
Pamoja na kumtembelea
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, miongoni mwa sehemu anazotarajiwa
kutembelea kama sehemu ya kujipatia uzoefu ni Chuo cha Uongozi wa
Mahakama Lushoto (IJA).
” Ninakwenda pia Lushoto na
pamoja na mambo mengine ninataka kuangalia uwezekano wa kuanzisha
ushirikiano na Chuo hicho kwa kuwaleta watu wetu na pia kuwaalika
wataalamu kutoka Chuo hicho kuja nchini Gambia”. amesisiza Jaji Mkuu
Jallow.
Kwa upande wake Mwanasheria Mkuu
ameunga mkono wazo la Jaji Mkuu la kuanzisha uhusiano wa karibu na
Chuo cha Uongozi wa Mahakama kwa kile alichosema ni moja ya Taasisi
muhimu sana katika utoaji wa mafunzo.
Akabainisha kuwa hata Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu nayo inaangalia namna bora zaidi ya kukitumia Chuo
katika kuwajenga uwezo na kuwapiga msasa wafanyakazi wa Ofisi yake.
Kuhusu maslahi na mazingira bora
ya kufanyia kazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali alisema ni eneo ambalo
linatakiwa kuangaliwa na kufanyiwa kazi.
“Maslahi ya wafanyakazi katika
sekta ya utoaji haki ni muhimu sana, na hasa ukizingatia kwa mfano
katika Ofisi yangu , wanafanya kazi kubwa, nzuri, kwa uadilifu na
uzalendo wa hali ya juu sana. Kuna haja na umuhimu wakuangalia pia
maslahi yao ili siyo tu kuwapa motisha ya kutekeleza majukumu yao
vizuri zaidi lakini pia kuwafanya wapende kubaki na kufanya kazi
serikalini. akaeleza Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Dk. Kilangi amemshukuru Jaji
Mkuu wa Gambia kwa kuitembelea Ofisi ya Mwanasheria Mkuu na
kubadilishana uzoefu na kwamba wakati wowote Ofisi hiyo itakuwa
tayari kushirikiana na Gambia kupitia sekta ya sheria na utoaji
haki.
Jaji Mkuu Hassan Jallow pia si
mgeni sana kwa Tanzania kwa sababu shahada yake ya kwanza ya Sheria
aliipata katika Chuo Kikuu cha Dar Es s Salaam ( 1973) na pia amewahi
kuwa Mwendesha Mashtaka wa iliyokuwa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji
ya Kimbari ya Rwanda ( ICTR) (2003-2015)
No comments:
Post a Comment