Na Florah Raphael.
Chama cha wananchi
CUF leo kimetoa maamuzi ya kikao cha kamati tendaji iliyokutana machi 25
mwaka huu katika ukumbi wa ofisi ya wabunge wa CUF uliopo magomeni, Dar
es salaam chini ya uenyekiti wa katibu mkuu.
Akiongea na vyombo
vya habari katibu wa chama hicho Seif Shairf Hamad amesema kuwa,katika
kikao hicho yalitolewa maamuzi mbalimbali kutokana na ajenda
zilizokuwepo mezani ambapo kuhusu ajenda ya uhujumu wa chama cha CUF
kamati iliamua chama kiendelee kufuatilia hujuma hizo kwa lengo la
kudhibiti pia iliagiza viongozi wa ngazi zote kuwa makini na kufuatilia
hila zote za kukihujumu chama na kuwafichua wale wote wanaopanga njama
hizo.
Aidha ameongeza kuwa
katika ajenda hiyohiyo waliamua kuwahimiza wanachama kuimarisha umoja,
ushirikiano na mshikamano huku wakitambua kuwa umoja ni silaha mujarabu
ya kuwashinda maadui wa chama.
Pia amesema kuwa
katika ajenda ya taarifa kuhusu maendeleo ya kesi za chama, kamati
inawapongeza mawakili wanaokiwakilisha chama katika kesi hizo kwa
kusimamia kwa dhati na kwa weledi wa hali ya juu na kuongeza kuwa kamati
inawaomba wanachama hasa wanaoishi jiji la Dar es salaam na viunga
vyake waendelee kujitokeza kwa wingi mahakamani kila siku ambayo kesi
inasikilizwa.
Kuhusu hali ya
usalama nchini Seif amesema kuwa kamati iliamua kuendelea kufuatilia kwa
makini malalamiko ya wananchi yanayotolewa kuhusu ukiukwaji wa haki zao
kisha kushauriana na wadau wote ikiwemo serikali ili kubaini ukweli wa
malalamiko hayo na kubaini chanzo chake ili kutokomeza kabisa hali
hiyo, kuikumbusha serikali kuwa jukumu lake la msingi ni kulinda usalama
wa raia na mali zao ili jeshi la polisi na vyombo vingine vya ulinzi
vijiimarishe kutimiza wajibu huo kwa weledi.
Pia ameongeza na
kusema kuwa kuhusu hali ya usalama nchini kamati pia iliamua
kuwakumbusha wananchi watimize wajibu wao na kutetea hali na kuhakikisha
kuwa Tanzania inaendelea kuwa na amani kwa kutofumbia macho vitendo
vyote viovu vinavyoweza kuitikisa misingi madhubuti ya taifa letu,
ikiwemo umoja na mshikamano.
Mwisho kamati ya
utendaji wa Taifa ilitoa wito kwa watanzania wote kuwa kitu kimoja
katika kutetea maslahi mapana ya nchi yetu na watu wake na kuendelea na
utamaduni wetu wa kuhurumiana na kushirikiana katika wakati wa majaribu
na wakati wa furaha.
Aidha Kutokana na
matokea hayo katibu wa CUF wilaya ya kinondoni mohamed s. Mikandu
ametoa malalamiko juu ya katibu wa chama hicho Seif Shairf Hamad
kufanya kongamano lililofanyika kata ya Tandare bila kumshirikisha na
kusema kuwa kongamano hilo halikuwa la chama bali walitumia jina la
chama ili kufanikisha malengo yao binafsi na kuongeza kuwa kongamano
hilo halikufuata utaratibu wa chama.
No comments:
Post a Comment